Kamendegere

(Elekezwa kutoka Pedetes)
Kamendegere
Kamendegere mashariki (Pedetes surdaster)
Kamendegere mashariki (Pedetes surdaster)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Anomaluromorpha (Wanyama kama kindi warukaji)
Familia: Pedetidae (Wanyama walio na mnasaba na kamendegere)
Gray, 1825
Jenasi: Pedetes
Illiger, 1811
Ngazi za chini

Spishi 2:

Kamendegere ni wanyama wakubwa kiasi wa jenasi Pedetes, jenasi pekee wa familia Pedetidae, ambao wanafanana na sungura wenye miguu ya nyuma mirefu au hata na kanguru mdogo, lakini hawana mnasaba na wanyama hawa. Rangi yao ni hudhurungi juu na nyeupe chini. Wanatokea nyika za Afrika ya Kusini na ya Mashariki[1][2]. Hukiakia usiku; wakati wa mchana hupumzika katika matundu yao ambayo wayachimba wenyewe. Hula mimea, mizizi na pengine wadudu. Jike huzaa mwaka mzima, mtoto mmoja kwa mara na mara tatu kwa mwaka.

Spishi

hariri

Spishi ya kabla ya historia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-01-17. Iliwekwa mnamo 2012-02-20.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-05. Iliwekwa mnamo 2012-02-20.
  3. Fossil Pedetidae (Rodentia) from Laetoli. Leakey, M.D.; Harris, J.M.[Eds]. Laetoli. A Pliocene site in northern Tanzania., Oxford University Press, Oxford, New York etc., 1987: i-xxii, 1-561. Chapter pagination: 171-190. [Zoological Record Volume 124]