Kamendegere
(Elekezwa kutoka Pedetidae)
Kamendegere | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kamendegere mashariki (Pedetes surdaster)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 2:
|
Kamendegere ni wanyama wakubwa kiasi wa jenasi Pedetes, jenasi pekee wa familia Pedetidae, ambao wanafanana na sungura wenye miguu ya nyuma mirefu au hata na kanguru mdogo, lakini hawana mnasaba na wanyama hawa. Rangi yao ni hudhurungi juu na nyeupe chini. Wanatokea nyika za Afrika ya Kusini na ya Mashariki[1][2]. Hukiakia usiku; wakati wa mchana hupumzika katika matundu yao ambayo wayachimba wenyewe. Hula mimea, mizizi na pengine wadudu. Jike huzaa mwaka mzima, mtoto mmoja kwa mara na mara tatu kwa mwaka.
Spishi
hariri- Pedetes capensis, Kamendegere Kusi (Springhare)
- Pedetes surdaster, Kamendegere Mashariki (East African Springhare)
Spishi ya kabla ya historia
hariri- Pedetes laetoliensis[3] (Pliocene ya Laetoli, Tanzania)
Picha
hariri-
Kamendegere kusi
-
Kamendegere kusi akiruka
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-01-17. Iliwekwa mnamo 2012-02-20.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-05. Iliwekwa mnamo 2012-02-20.
- ↑ Fossil Pedetidae (Rodentia) from Laetoli. Leakey, M.D.; Harris, J.M.[Eds]. Laetoli. A Pliocene site in northern Tanzania., Oxford University Press, Oxford, New York etc., 1987: i-xxii, 1-561. Chapter pagination: 171-190. [Zoological Record Volume 124]