Kunguni-mgunda

(Elekezwa kutoka Pentatomomorpha)
Kunguni-mgunda
Kisulisuli mraba-mweusi (Dysdercus nigrofasciatus)
Kisulisuli mraba-mweusi (Dysdercus nigrofasciatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Heteroptera
Oda ya chini: Pentatomomorpha
Leston, Pendergrast & Southwood, 1954
Ngazi za chini

Familia za juu 5:

Kunguni-mgunda ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda ya chini Pentatomomorpha katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa) ambao wana mabawa ya mbele yaliyo nusu magumu na nusu kama kiwambo. Takriban wadudu hao wote hufyonza utomvu wa mimea, matunda au mbegu, lakini spishi nyingine hula kuvu na nyoga au wadudu wadogo. Spishi fulani huitwa visulisuli pia.

Mifano ya wadudu hao ni kunguni-ngao (familia Pentatomidae), kunguni-bapa (familia Aradidae), kunguni-mbegu (familia Lygaeidae na Rhyparochromidae) n.k.

Maelezo

hariri

Miundo na ukubwa ya kunguni-mgunda yanatofautana sana. Lakini, sifa zao ni sehemu za mdomo zinazotoboa ili kufyonza vioevu na mabawa ya mbele yaliyo nusu magumu na nusu kama viwambo. Takriban spishi zote hufyonza utomvu kutoka mashina, matunda na mbegu. Spishi chache kiasi hujilisha kwa wadudu wadogo au kuvu.

Kama wadudu mabawa-nusu wote lava za Pentatomomorpha zinafanana na wapevu. Kwa kawaida kuna hatua tano na ile ya mwisho inaambua kuwa mpevu mara moja bila kupita kwa hatua ya bundo. Mayai hutagwa juu ya mimea mara nyingi. Spishi za Aradoidea zinataga chini ya gome la miti au chini ya takataka ya majani. Spishi fulani hubeba mayai mgongoni.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Anoplocnemis curvipes (Coreidae)
  • Antestiopsis thunbergii (Pentatomidae)
  • Clavigralla tomentosicollis (Coreidae)
  • Dysdercus cardinalis (Pyrrhocoridae)
  • Dysdercys fasciatus (Pyrrhocoridae)
  • Dyscerdus nigrofasciatus (Pyrrhocoridae)
  • Geocoris ruficeps (Lygaeidae)
  • Oxycarenus hyalinipennis (Lygaeidae)
  • Probergrothius angolensis (Pyrrhocoridae)
  • Pseudotheraptus wayi (Coreidae)
  • Usambaraia ampliata (Aradidae)