Peroksidi ya hidrojeni
Peroksidi ya hidrojeni (kwa Kiing. hydrogen peroxide) ni kampaundi ya kikemia inayofanywa na hidrojeni na oksijeni. Fomula yake ni H2O2. Ni kioksidishaji kikali kinachotendana sana na dutu mbalimbali. Hutumika kama dawa ya kusafisha na ya kuondoa rangi kwenye nywele.
Hutumiwa pia kama fueli ya roketi.
Kwa ukolezi wa 3% (ikimaanisha kuwa kuna gramu 3 za peroksidi ya hidrojeni kwa gramu 100 za maji), inaweza kutumika kutibu majeraha.
Baada ya muda itatengana polepole kuwa gesi ya oksijeni na maji.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Peroksidi ya hidrojeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |