Ghuba ya Uajemi

(Elekezwa kutoka Persian Gulf)

Ghuba ya Uajemi (Kiajemi: خلیج فارس khalij-e fārs; Kiarabu: الخليج الفارسي al-khalīj al-fārsī; pia: الخليج العربي al-khalīj al-ʿarabī „Ghuba Arabu“) ni ghuba kubwa la Bahari Hindi kati ya Uajemi na rasi ya Uarabuni.

Ramani ya Ghuba ya Uajemi

Inaanza kwenye Mlango wa Hormuz na kuendelea hadi mwisho wake upande wa Kuwait na mdomo wa Shatt al Arab.

Ni kawaida ya kuiita ghuba ya Uajemi lakini katika fitina ya miaka iliyopita nchi kadhaa za Waarabu ziliita "Ghuba Arabu". Zamani iliitwa pia "Ghuba ya Basra" na hili ndilo jian lake hadi leo katika lugha ya Kituruki "Basra Körfezi).

Nchi jirani

Nchi zinazopakana na ghuba ni:

Umuhimu wa kisiasa na kiuchumi

Nchi za ghuba zimekuwa muhimi sana duniani kwa sababu ya mafuta ya petroli inayopatikana hapa kwa wingi. Utajiri huu umebadilisha uso wa nchi zinazopakana na ghuba.

Utajiri huo umesababisha pia vita kadhaa kama vile vita ya Iran-Iraq, vita ya Iraq-Kuwait, vita ya ghuba.

Jiografia

Eneo lote la ghuba ni 233,000 km². Maji matamu huingia kwa njia ya mito ya Frati na Hidekeli inayoungana katika Shatt al Arab.

Urefu wake ni takriban 1,000 km na upana wake kati ya 200 hadi 300 km. Kina hakizidi 100 m.

Mlango wa Hormuz unaunganisha ghuba na Bahari Arabu ambayo ni bahari ya kando ya Bahari Hindi.