Peterson Munuhe Kareithi

Peterson Munuhe Kareithi alikuwa mwandishi, mwalimu na mwanasiasa wa nchi ya Kenya.

Maisha ya awali hariri

Alizaliwa kwenye kijiji cha Mbari-ya-Hwai, katika Kaunti ya Nyeri.

Alisomea shule ya Tumutumu na hatimaye kwenda shule ya Kagumo TTC, ambapo alihitimu kupata shahada ya ualimu wa shule za msingi. Alianza kufundisha mnamo 1954 huku akijieleimisha mwenyewe, na mwishowe akapata nafasi ya kuingia Chuo Kikuu cha Makerere. Baadaye, alienda kusoma Chuo cha Kent, Ohio, iliyoko Marekani.

   "Omite ta Kariithi" ni tashbihi ya lugha ya Kikuyu inayosema "Amejipamba kama Kariithi". Kariithi alirudi kutoka   ngambo akiwa amejitwika suti maridadi sana.

Uandishi hariri

Munuhe alipata umaarufu baada ya kuchapisha kitabu chake "Kaburi Bila Msalaba" mnamo 1969. Katika kitabu hicho, anatoa kumbukumbu ya mambo aliyoshuhudia wakati wa Hali ya Hatari kabla Kenya haijajinyakulia uhuru. Kitabu hicho kimetafsiriwa hadi lugha ya Kiingereza.

Siasa hariri

Munuhe aliwania ubunge wa Mathira mnamo 1974 lakini alishindwa na Davidson Ngibuini Kuguru. Enzi hizo, alikuwa katika kikundi cha kisiasa cha vijana kilichokuwa kikiongozwa na J.M. Kariuki waliosoma na ambao walitaka kuikomboa nchi kutoka uongozi wa wanamgambo ("homeguards").[1] Hata hivyo, alipata kazi katika ofisi za Wizara ya Elimu kule Jogoo House.

Kifo hariri

Alifariki mwezi Juni mwaka wa 1977 katika ajali ya gari eneo la Kenol Junction, karibu na Kabati. Lori la kubeba mawe ya ujenzi liligonga gari lake. Hii ilitokea kabla ya uchaguzi wa 1977.

Tanbihi hariri

  1. "Kenol black spot snuffs out ambitions of visionary Gakuru - Daily Nation". web.archive.org. 2019-07-30. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-30. Iliwekwa mnamo 2019-07-30. 

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peterson Munuhe Kareithi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.