Pirenei
(Elekezwa kutoka Pyrenees)
Pirenei (Kifaransa: Pyrénées; Kihispania: Pirineos) ni safu ya milima katika Ulaya ya kusini-magharibi inayotenganisha nchi za Ufaransa na Hispania. Zina urefu wa kilomita 430 kati ya bahari ya Atlantiki na bahari ya Mediteranea.
Pirenei za kati ni sehemu ya juu kuna milima 200 yenye kimo cha zaidi ya mita 3000. Mingi ina barafu na theluji ya kudumu hata kama barafuto zinarudi nyuma. Milima mikubwa ni hasa
- Pico d'Aneto au Pic de Néthou yenye mita 3,404
- Mont Posets yenye mita 3,375
- Mont Perdu au Monte Perdido au Mont Perdut ("mlima uliopotea") 3,355 m (11,007 ft).
Katika historia Pirenei zilikuwa kizuizi cha usafiri hivyo pia mpaka muhimu wa kisiasa. Mipito ni michache tena mikali. Katikati ya milima iko utemi wa Andorra iliyobaki kama nchi ya pekee kwa sababu ya tabia ya milima iliyozuia nchi kubwa jirani zisiimeze.
Tovuti za Nje
hariri- Great Routes: Pirineos Archived 2012-12-18 at Archive.today, from a website of the Instituto de Turismo de España
- Official website Archived 5 Machi 2006 at the Wayback Machine. of France's Pyrenees National Park
- Photos of Pyrenees Archived 5 Desemba 2005 at the Wayback Machine. from a geodynamics researcher at the University of Washington
- Cycling the French High Pyrenees and Ariege Pyrenees photos and video by steephill.tv bike travelogue
- The Aude and Pyrénées-Orientales Online resource for the Aude & Pyrénées-Orientales departments of the Languedoc-Roussillon.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Pirenei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |