Kwelea

(Elekezwa kutoka Quelea)
Kwelea
Kwelea domo-jekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Jenasi: Quelea
Reichenbach, 1850
Ngazi za chini

Spishi 3:

Kwelea ni ndege wadogo wa jenasi Quelea katika familia Ploceidae ambao wanatokea Afrika. Wanafanana na kwera lakini hawana rangi ya manjano. Rangi zao ni kahawia na michirizi myeusi juu na nyeupe au pinki chini na wana kichwa, kidari na/au domo nyekundu au pinki. Ndege hawa hula mbegu hasa lakini wadudu pia, hususa makinda madogo. Hulifuma tago lao kwa majani ya manyasi na hulining'inizia kitawi. Matago yao hupatikana katika makundi makubwa. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi

hariri