Regional Internet Registry
Regional Internet Registry (kifupi: RIR; kwa Kiswahili: Usajili wa intaneti wa kikanda) ni jina la taasisi zinazosimamia ugawaji na usajili wa anwani za internet ndani ya kanda fulani ya Dunia.
Miongoni mwa namba wanazoshughulikia mna anwani za IP (zote: IPv4 na IPv6) na mfumo wa namba za kujitegemea (kwa matumizi ya kupanga taratibu nzima za BGP, yaani, jinsi ya kugawa mifumo ya mitandao kwa mpangilio, mitandao ya simu, data electronikia na vilevile Internet).
Orodha ya usajili wa internet kikanda
haririSasa kuna RIRs tano katika operesheni:
- American Registry for Internet Numbers (ARIN) [1] kwa Amerika Kaskazini na sehemu za Karibi
- RIPE Network Coordination Centre (RIPE NCC) [2] kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia ya Kati
- Asien-Pacific Network Information Centre (APNIC) [3] kwa ajili ya Asia-Pasifiki
- Latin American and Caribbean Internet Addresses Registry (LACNIC) [4] kwa Amerika ya Kusini na maeneo ya kanda ya Karibi
- African Network Information Centre (AfriNIC) [5] kwa ajili ya Afrika
Uhusiano kati ya RIRs na IANA
haririMamlaka ya Usajili wa Namba za Internet (kwa Kiingereza: Internet Assigned Numbers Authority au IANA) inasimama kama mwakilishi wa idadi ya namba za Internet kwa RIRs, halafu, kwa kufuata sera za ugawaji wa namba katika kanda kwa wateja wao, ambao pia inawajumlisha watoa huduma ya Internet, yaani, "Internet service provider" - halafu wao hutoa huduma hiyo kwa masharika au watu binafsi. Kwa pamoja, RIRs nao hushirkiana na Number Resource Organization (NRO),[6] iliundwa kama bodi wakilishi kwa ajili ya kukusanya mapato yao, kumaliza shughuli za kimuungano, na kueneza shughuli zao kimataifa. NRO imeingia mkataba na ICANN kwa ajili ya kuanzisha "Address Supporting Organisation"(ASO), yaani, Shirika la Kusaidia Anwani za Mtandao[7] ambalo lenyewe linashughulikia sera ya kimataifa ya anwani za IP ikiwa ndani ya sehemu ya kazi za ICANN.
Uondoaji wa anwani za ipv4
haririAnwani za ipv4 zinazogawiwa kwa watumiaji zakaribia kuisha. Hili lilikadiriwa miaka mingi kwani kwa sasa anwani zaidi ya bilioni nne zimepewa watu na haswa mashirika. Mashirika na makampuni mengi yalichukua anwani nyingi kuliko vile walizokuwa wakizihitaji. Kwa njia hii ili kusiwe na upungufu wa anwani hizi, huenda shirika la ugavi wa anwani hizi IANA wakafanya haya:
- Shirika zilizo na anwani nyingi kuliko vile wanahitaji waitishwe.
- Ikiwa shirika fulani halitafuata sheria za anwani hizi, huenda wakaitishwa
- Ugavi waweza kurudiwa tena ili kila shirika linalohitaji anwani hizi wapewe wanazofaa [8].
Ikiwa anwani hizi zitaendelea kupungua anwani mpya za ipv6 zitagawiwa kwa wale wanaofaa.
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
hariri- Kanda 5 za usajili wa intaneti
- ARIN - American Registry for Internet Numbers Archived 19 Agosti 2018 at the Wayback Machine. - Amerika Kaskazini na Karibi
- RIPE NCC - RIPE Network Coordination Centre - Ulaya, the Mashariki ya Kati na Asia ya Kati
- APNIC - Asia-Pacific Network Information Centre Asia na Pacific region
- LACNIC - Latin American and Caribbean Internet Address Registry - Amerika Kusini na Karibi
- AfriNIC - African Network Information Centre - Afrika
- Vingine
- Internet Corporation kwa kupewa majina na idadi (ICANN)
- Idadi Resource Organization (NRO)
- ipv4 depletion Archived 19 Agosti 2018 at the Wayback Machine.
- IPv4 Address
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Regional Internet Registry kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |