Raphael S. Ndingi Mwana a'Nzeki
Raphael S. Ndingi Mwana a'Nzeki (Mwala, Kenya, 25 Desemba 1931 - 31 Machi 2020) alikuwa askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi nchini Kenya[1].
Maisha
haririMwana a'Nzeki alipadrishwa tarehe 31 Januari 1961 na askofu John Joseph McCarthy mjini Nairobi. Tarehe 29 Mei 1969 aliwekwa wakfu kuwa askofu wa Machakos. Tarehe 30 Agosti alikuwa askofu wa Nakuru.
Mwaka 1996 aliitwa kuwa msaidizi wa askofu mkuu wa Nairobi kardinali Maurice Otunga akamfuata Otunga katika nafasi ya askofu mkuu tarehe 21 Aprili 1997.
Baada ya kutimiza umri wa miaka 75 alikubaliwa kustaafu na Papa Benedikto XVI akafuatwa madarakani na John Njue aliyewahi kuwa msaidizi wake huko Nakuru.
Viungo vya Nje
hariri- ↑ Retired Catholic Archbishop Mwana a'Nzeki dies in Nairobi, Daily Nation tar. 1 -04-2020