Machakos
Machakos ni mji wa Kenya (Ukambani) takriban kilomita 64 upande wa kusini-mashariki wa Nairobi. Ni makao makuu ya kaunti ya Machakos.
Machakos | |
Mahali pa mji wa Machakos katika Kenya |
|
Majiranukta: 1°31′0″S 37°16′0″E / 1.51667°S 37.26667°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti za Kenya | Machakos |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 150,041 |
Machakos imekua haraka kwa sababu ni karibu na mji mkuu wa taifa imeshapita idadi ya wakazi lakhi moja na nusu[1]. Wenyeji wa Machakos ni hasa Wakamba.
Historia
haririMachakos ni kati ya miji ya kwanza ya Kenya bara ikaundwa mwaka 1899 na Waingereza na kuwa makao makuu ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (mbali na eneo lindwa la pwani lililokodishwa na Usultani wa Zanzibar na Uingereza) kwa muda mfupi.
Jina la mji lilitokana na chifu Masaku wa Wakamba aliyewahi kuwa na boma lake hapo.
Baada ya azimio la kutounganisha Machakos na reli ya Uganda mji haukuendelea sana.
Mwaka 2002 majadiliano kati ya pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan yalifanyika Machakos.
Kituo kikuu cha mabasi mjini Nairobi huitwa na wenyeji "Machakos Country Bus".
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Viungo vya nje
hariri- Habari za historia ya Wakamba
- Habari za mlima Kituluni karibu na Machakos Archived 15 Januari 2010 at the Wayback Machine..
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Machakos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |