Rena Callist
Rena Callist Nyamwelo (amezaliwa 24 Machi 1971) ni mjasiriamali, msimamizi wa wanamitindo, mratibu wa matamasha mbalimbali hasa muziki wa kizazi kipya na dansi, na mkereketwa wa burudani kindakindaki kutoka nchini Tanzania. Rena pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kings & Queens Worldwide Co. Limited, Rena Events Limited, Kibara Mining Limited na Digital AM Limited.
Mwaka wa 1993, alikuwa miongoni mwa Watanzania wa mwanzo kuanzisha mashindano ya urembo nchini kwa kuandaa mashindano ya Miss Coca-Cola.
Rena Callist ni mwanzilishi na mmiliki wa mashindano ya urembo ya Miss East Africa aliyoyaanzisha mwaka 1996. Pia huratibu mashindano ya walimbwende wa Afrika Mashariki.[1] Vilevile alisimamia onesho kubwa la disko lililofanyika mwaka 1994 kwa minajili ya kuchangia pesa kwa ajili ya hayati DJ Kalikali (Tanzania DJS Festival).
Mwaka wa 1997 aliwaleta tena watu pamoja katika onesho la "Full Blast Music Show" iliyofanyika jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL).
Wanamuziki kutoka nje ambao aliwahi kusimamia ujio wao kwa Tanzania ni pamoja na Lucky Dube (1997), Yvone Chakachaka.
Marejeo
hariri- ↑ "Home » Entertainment". www.thisday.co.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-25. Iliwekwa mnamo 2021-04-25.
{{cite web}}
: no-break space character in|title=
at position 5 (help)
Viungo vya nje
hariri- Rena Callist katika Instagram