Lucky Dube
Lucky Philip Dube (tamka doo-bei) [1] (3 Agosti 1964 - 18 Oktoba 2007) alikuwa mwanamuziki wa reggae kutoka Afrika Kusini. Alirekodi albamu 22 katika lugha ya Kizulu, Kiingereza na Kiafrikaans katika kipindi cha miaka 25 na alikuwa mwanamuziki wa Reggae kutoka Afrika Kusini ambaye aliuza albamu nyingi kabisa. [2] [3] Dube aliuawa katika kitongoji cha Rosettenville huko Johannesburg jioni ya 18 Oktoba, mwaka 2007. [3] [4] [5]
Lucky Dube | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Lucky Philip Dube |
Amezaliwa | Ermelo, Transvaal (now Mpumalanga), Afrika Kusini | Agosti 3, 1964
Amekufa | 18 Oktoba 2007 (umri 43) Rosettenville, Johannesburg Gauteng, South Africa |
Aina ya muziki | reggae, mbaqanga |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Ala | Sauti, Kinanda |
Miaka ya kazi | 1982 - 2008 |
Studio | Rycodisc, Gallo Record Company |
Ame/Wameshirikiana na | The Love Brothers |
Tovuti | Official website |
Wasifu wake
haririMaisha Yake ya Utotoni
haririLucky Dube alizaliwa Ermelo, zamani lilikuwa eneo la Transvaal ya Mashariki, na sasa ni sehemu ya Mpumalanga, tarehe 3 Agosti mnamo mwaka 1964. Wazazi wake walitalikiana kabla ya yeye kuzaliwa na alilelewa na mama yake, Sarah, ambaye alimpa jina hilo kwa sababu alichukulia kuzaliwa kwake kama bahati baada ya mimba nyingi kutoka/kuharibika. [6] Pamoja na ndugu zake wawili, Thandi na Patrick, kwa kipindi cha muda mrefu utotoni mwake Dube aliishi na nyanyake/bibi yake, wakati mama yake alihamishwa kufanya kazi sehemu nyingine. Kwenye mahojiano ya mwaka 1999 alimsimulia nyanyake/bibi yake kama "mpenzi wake wa dhati" ambaye "alizidisha vitu vingi kumkuza kuwa mtu wa kuwajibika aliye sasa." [7] [8]
Kuanza Uwanamuziki wake
haririUtotoni mwake Dube alilima lakini, alipokuwa mtu mzima, na kutambua kwamba hakuchuma pato la kumwezesha kulisha familia yake, alianza kuenda shuleni. Akiwa shuleni alijiunga na kwaya, pamoja na marafiki wengine, na kuunda kikundi chake cha kwanza cha waimbaji kilichoitwaThe Skyway Band. [8] Alipokuwa shuleni aligundua kuhusu harakati za Rastafara. Akiwa na umri wa miaka 18 Dube alijiunga na bendi ya binamu yake, The Love Brothers, iliyoimba muziki wa pop kwa lugha ya Kizulu zilizojulikana kama mbaqanga huku akiyakimu maisha yake kwa kufanya kazi na kampuni ya Hole and Cooke kama mlinzi kwenye mnada wa magari huko Midrand. Bendi hiyo iliinga kwenye mkataba na kampuni ya Teal Record, chini ya Richard Siluma (Baadaye Teal iliunganishwa na Kampuni ya Gallo Record). Ingawa bado Dube alikuwa shuleni, bendi hiyo ilirekodi katika mji wa Johannesburg wakati alikuwa likizoni. Albamu waliotoa iliitwa kwa jima la Lucky Dube and the Supersoul. Albamu ya pili ilitolewa muda mchache baadaye, mara hii kando na kuimba Dube alitunga misitari. Ni wakati huu ambao alianza kujifunza Kiingereza. [8]
Kuhamia rege
haririBaada ya kwa albamu yake ya tano ya Mbaqanga, Dave Segal (ambaye badaye alikuwa mhandisi wa sauti ya Dube) alimshauri aachane na jina la "Supersoul". Albamu zingine zote zilizofuata zilirekodiwa kama Lucky Dube. Wakati huu Dube alianza kugundua kwamba mashabiki walifurahishwa na baadhi ya nyimbo za rege alizoimba hadharani. Aliweza kuvutiwa na Jimmy Cliff [9] na Peter Tosh, [7] alihisi kwamba ujumbe wa masuala ya kijamii na kisiasa uliohusishwa na rege ya kutoka Jamaica ungefaa kwa hadhira ya Afrika Kusini jamii ambayo ubaguzi wa rangi(usarangi) ulikuwa umekithiri. [9]
Aliamua kujaribu mtindo huu mpya wa muziki na katika mwaka wa 1984, alitoa albamu ndogo ya Rastas Never Die. Mauzo ya rekodi hiyo yalikuwa mabaya - idadi ilikuwa karibu 4000- ikilinganishwa na 30000 ambayo rekodi yake ya mbaqanga zingeuzwa. Serikali iliyoeneza usarangi (ubaguzi wa rangi), ikiwa na nia ya kukomesha harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, ilipiga marufuku albamu hiyo mwaka 1985. [10] Hata hivyo, hakuvunjika moyo na aliendelea kuimba nyimbo za rege hadharani na akatoa albamu ya pili ya rege. Think About The Children (1985). Ilifanikiwa kupata hali ya mauzo ya zaidi ya milioni na kumfanya Dube kuwa mwanamziki wa rege maarufu Afrika Kusini, mbali na kuvutia watu nje ya nyumbani kwao. [8]
Mafanikio muhimu na ya kibiashara
haririDube aliendelea kutoa albamu zilizofanikiwa kibiashara. Mwaka 1989 alishinda tuzo nne za OKTV wimbo wa Prisoner, ulishinda nyingine na wimbo wa Captured Live ulishinda tuzo nyingine mwaka uliofuata na bado wimbo wa House Of Exile ulishinda tuzo mbili mwaka mmoja baadaye. [11] Albamu yake ya mwaka 1993, Victims iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. [2] Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi duniani na na kampuni ya Motown. Albamu yake ya Trinity ilikuwa ya kwanza kutolewa na kampuni ya Tabu Records baada ya Motown {1{/1} kujipatia kitambulisho hicho. [11]
Mnamo mwaka 1996 alitoa mkusanyiko albamu ya, Serious Reggae Business, ambayo ilimpelekea kuitwa "Mwanamziki wa Kiafrika mwenye mauzo bora zaidi" kwenye Tuzo la Wanamziki Duniani na "Msanii bora wa Mwaka" kwenye Tuzo la Wanamziki nchini. Albamu zake tatu zilizofuata zote zilishinda tuzo kwenye Tuzo la Wanamziki la Afrika Kusini. [11] Albamu yake ya hivi karibuni, Respect, ilipata nafasi ya kutolewa Ulaya na Kampuni ya Muziki ya Warner Musi. [2] Dube alizuru nchi nyingi, na kuimba kwenye jukwaa moja na wasanii kama vile Sinéad O'Connor, Peter Gabriel na Sting. [9] Alishiriki kwenye igizo la rege liitwalo Sunsplash mwaka 1991 (hali ya kipekee mwaka huo, alialikwa jukwaani tena na kuimba kwa muda wa dakika 25 akirudia) na onyesho la hadharani la 8 la mwaka 2005 mjini Johannesburg. [9]
Mbali na kuimba, wakati mwingine dube alikuwa muigizaji, alishiriki kwenye filamu za Voice In The Dark, Getting Lucky na Lucky Strikes Back. [12]
Kifo
haririLucky Dube aliuawa katika kitongoji cha Rosettenville mjini Johannesburg tarehe 18 Oktoba 2007, muda mfupi baada ya kuwapeleka watoto wake wawili kati ya wote saba kando ya nyumba ya mjomba wao. |18 Oktoba 2007, muda mfupi baada kuwapeleka watoto wake wawili kati ya wote saba kando ya nyumba ya mjomba wao. [13]]] Dube alikuwa akiendesha gari lake la aina ya Chrysler 300C ambayo kumbe ndiyo wauaji wake walikuwa wanataka. Duru za polisi zinaonyesha kuwa aliuawa kwa kupiga risasi na wezi wa magari. Wanaume watano wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo [14] Watu watatu wwalishitakiwa na kupatikana na hatia tarehe 31 Machi 2009; wawili walijaribu kutoroka lakini walishikwa. [15] Watu hao walihukumiwa kifungo cha maisha. [16]
Aliacha mjane Zanele na watoto wake saba.
Hiba
haririTarehe 21 Oktoba 2008, Rykodisc alitoa albamu ya mkusanyiko kwa jina Retrospective, ambayo ilikuwa na nyimbo nyingi za kuvutia za Dube pamoja na traki nyingine ambazo hazikuwa zimetolea vilevile awali unreleased tracks katika Marekani. Albamu hiyo ilisifia muziki wa Dube na kuadhimisha mchango aliyotoa nchini Afrika ya Kusini. [17]
Diskografia
hariri- Lengane Ngeyethu (1981)
- Kudala Ngikuncenga (1982)
- Kukuwe (1983)
- Abathakathi (1984)
- Ngikwethembe Na? (1985)
- Umadakeni (1987)
- Help My krap (1986)
- Rastas Never Die (1984)
- Think About The Children (1985)
- Slave (1987)
- Together As One (1988)
- Prisoner (1989)
- Captured Live (1990)
- House of Exile (1991)
- Victims (1993)
- Trinity (1995)
- Serious Reggae Business (1996)
- Tax Man (1997)
- The Way It Is (1999)
- Ili The Rough Guide Lucky Dube (mkusanyiko) (2001)
- Soul Taker (2001)
- The Other Side (2003)
- Respect (2006)
- The Best Lucky Dube wa (2008)
- Lucky Dube Live In Uganda (2008)
- Retrospective (2008)
Viungo vya nje
hariri- tovuti rasmi Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Diskogradfia rasmi - Discogs
Marejeo
hariri- ↑ Fun Facts, luckydubemusic.com, ilitolewa tarehe 19 Oktoba 2007
- ↑ 2.0 2.1 2.2 [2] ^ Five facts about raggae star Lucky Dube, Reuters, tarehe 19 Oktoba 2007
- ↑ 3.0 3.1 [3] ^ S. Africa reggae icon shot and killed - radio, Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. Reuters, tarehe 19 Oktoba 2007.
- ↑ Hijackers gun down Lucky Dube, Ilihifadhiwa 28 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. News24.com, tarehe 19 Oktoba 2007
- ↑ S African reggae star shot dead, BBC News, tarehe 19 Oktoba 2007
- ↑ Car jacker kills reggae star, CNN, tarehe 19 Oktoba mnamo mwaka 2007.
- ↑ 7.0 7.1 [8] ^ Luvuyo Kakaza, Getting Lucky, Ilihifadhiwa 11 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. The Mail & Guardian, tarehe 26 Agosti 1999.
- ↑ 8.0 8.1 8.2 8.3 Finding reggae, Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. luckydubemusic.com, ilitolewa tarehe 19 Oktoba mnamo mwaka 2007
- ↑ 9.0 9.1 9.2 9.3 [12] ^ Basildon Petain, South African raggae star shot dead in front of his chilldren, Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. The Independent, tarehe 19 Oktoba 2007.
- ↑ condolences pour in for Lucky Dube, Ilihifadhiwa 21 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. SABC, 19 Oktoba 2007.
- ↑ 11.0 11.1 11.2 [17] ^ Discography, Ilihifadhiwa 27 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine. luckydubemusic.com, ilitolewa tarehe 19 Oktoba 2007
- ↑ Who's Who: Lucky Dube, Ilihifadhiwa 23 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine. News24, ilitolewa tarehe 10 Oktoba 2007
- ↑ Bobb, Scott. "S. African Reggae Star Lucky Dube Killed in Attempted Car-Jacking", VOA News, Voice of America, 19 Oktoba 2007. Retrieved on 2 Januari 2009. Archived from the original on 2008-01-06.
- ↑ "Five arrests over SA star's death", BBC News, 21 Oktoba 2007.
- ↑ Three Accused of the Murder of Lucky Dube Found Guilty Habari za Yahoo, 31 Machi 2009
- ↑ Reggae Star's Killers Get Life Habari za Yahoo, tarehe 2 Aprili 2009
- ↑ Lucky Dube - Bio|Artist|RYKODISC Ilihifadhiwa 1 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.