Riyad Mahrez
Riyad Karim Mahrez (alizaliwa 21 Februari 1991) ni mchezaji wa kulipwa wa soka ambaye anacheza kama winga katika klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City na timu ya taifa ya Algeria.
Mahrez alianza kazi yake kama mchezaji wa vijana wa klabu ya Ufaransa AAS Sarcelles. Ambapo alicheza kwa msimu mmoja tu kabla ya kuhamia Le Havre, akitumia muda wa miaka mitatu pamoja nao.
Mnamo Januari 2014, Mahrez alisaini mkataba na klabu ya Uiingereza Leicester City, aliisaidia Leicester city kushinda michuano mbalimbali.
Alizaliwa nchini Ufaransa, Mahrez alicheza mechi yake ya kimataifa na Algeria mwaka 2014 na aliiwakilisha kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2014 na Kombe la Mataifa ya Afrika 2015 na 2017. Mnamo mwaka wa 2016 aliitwa Mchezaji bora wa Afrika na CAF.
Mnamo tarehe 10 Julai 2018, Manchester City ilithibitisha kusainiwa kwa Mahrez kwa mkataba wa miaka mitano. Ada ya uhamisho wake ulikuwa £ milioni 60. Ada hiyo ilimfanya Mahrez awe mchezaji wa thamani kubwa kuliko wote Afrika.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Riyad Mahrez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |