Roger Scott
Roger Scott (23 Oktoba 1943 - 31 Oktoba 1989) alikuwa Mwingereza aliyecheshimiwa sana katika sekta ya redio. Alikuwa mchaguzi na mchezaji nyimbo katika stesheni za redio. Alifahamika sana kwa kuwasilisha kipindi cha alasiri katika stesheni ya redio ya London,Capital Radio,tangu mwaka wa 1973 hadi mwaka wa 1988.
Alizaliwa jijini London katika mwaka wa 1943, Roger Scott alikuza upendo wa nyimbo za aina ya rock na roll zilizokuwa zikitungwa katika mwisho wa miaka ya 1950 na mapema miaka ya 1960. Akiwa kijana, alianza kucheza muziki karibu na dirisha ya nyumba yao jijini London na kuangalia hisia za wapita njia kwa muziki alizocheza.
Wasifu wa Mapema
haririBaada ya muda mfupi kama mfanyibiashara wa baharini,Scott alipata njia na akaingia nchini Marekani na akajiunga na stesheni ya redio ya WPTR ya Albany,New York katika mwaka wa 1966. Kazi ya Scott,kwa sababu ya lafudhi yake ya Uingereza,ilikuwa kuwa 'rafiki wa Beatles' na hapo ndipo Scott akaanza kujifunza kazi ya kuwa mchezaji wa muziki kama DJ akifanya kazi na Boom Boom Brannigan na watu wengine maarufu wa stesheni hiyo. Miezi minane baadaye,alitoka WPTR kuwasilisha kipindi cha jioni katika stesheni ya Montreal ya 1470 CFOX. Kutoka mwaka wa 1967 hadi mwaka wa 1971 akapendwa katika stesheni hiyo kwa mitindo yake ya uwasilishaji na upendo wake wa dhati wa muziki. Hasa wakati huu alishiriki katika Give Peace A Chance iliyorekodiwa na John Lennon na Yoko Ono walipokuwa katika Hoteli ya Queen Elizabeth jijini Montreal.
Akitarajia uzinduzi wa stesheni za kibiashara za redio,Scott alirudi Uingereza katika mwaka wa 1971,lakini akapata maendeleo hayakuwa mbele kama alivyofikiri. Wakati uo huo, yeye alipata nafasi ya kazi katika UBN,stesheni ya kampuni ya United Biscuits, iliyotangaza habari kwa viwanda vya kampuni hiyo katika taifa zima. Ilikuwa wakati huu ,pia, alifanya kazi katika stesheni ya BBC Redio lakini akingoja kazi ya baadaye katika redio ya kibiashara alifanya kazi hiyo chini ya jina "Bob Baker."
Wasifu
haririCapital Radio
haririRedio za kibiashara ,hatimaye,zilipewa mamlaka katika mwaka wa 1972 na katika mwaka wa 1973 alijiunga na wafanyikazi wa stesheni ya London,Capital Radio. Vipindi vya alasiri vya Scott vikapata umaarufu sana baina ya wakazi wa London, akizalisha vipindi maarufu kama Three O'Clock na Hitline pamoja na wimbo wa Grab a a little piece of heaven ulioimbwa na David Dundas. Katika mwaka wa 1976, kipindi chake cha mara kwa mara cha Ijumaa cha kucheza nyimbo za kitambo kilipata mashabiki wa dhati. Hasa,kwa sababu ya Scott kuchezesha nyimbo zisizojulikana za aina ya rock-a-billy kwa mara ya kwanza.
Scott hakufuata orodha za kawaida za muziki , utafiti wowote wa wasikilizaji ama mbinu zozote za stesheni za kibiashara katika miaka ya 1980.Alitumia mbinu zake.
Radio 1
haririKatika mwezi wa Juni 1988,baada ya miaka kumi na mitano katika Capital, alihamia stesheni isiyo ya kibiashara ya BBC Radio 1. Akiwa huko,alifikia wasikilizaji wa taifa zima kwa mara ya kwanza,akiwasilisha kipindi cha alasiri cha Jumamosi na kipindi cha usiku cha Jumapili. Katika kipindi cha Jumamosi,alihusisha mahojiano na wanamuziki maarufu wengi kama Dion,Jackson Browne,Don Henley na wengine wengi. Vipindi vyake vya Jumapili vimekuwa vya kufurahisha hasa ikishirikisha muziki ya rock na roll ya miaka ya 1950 na muziki ya aina nyingi.
Roger Scott aliaga dunia katika mwaka wa 1989,akiwa umri wa miaka wa 46, baada ya kuugua kansa kwa muda mfupi.
Marejeo
haririmarejeo haya yako katika lugha ya Kiingereza