Jioni (yaani "kwenye jio" la usiku) ni kipindi cha siku karibu na machweo ambako mwanga wa mchana unazidi kupungua hata kuingia kwa giza la usiku.

Kutwa huko Coquitlam, British Columbia, Canada.

Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati wa kuacha shughuli mbalimbali na kujiandaa kwa usingizi, ingawa uenezi wa taa umebadilisha sana ratiba ya watu wengi.

Katika dini mbalimbali, ni wakati muhimu wa sala.

Katika kalenda ya Kiyahudi na kalenda ya Kiislamu jioni ni mwisho wa siku na kuanzia machweo ni mwanzo wa siku mpya, tofauti na hesabu sabifu ya kimataifa inayohesabu siku mpya kuanzia "katikati ya usiku" yaani saa sita usiku (24.00 h au 0.00 h)

Alfajiri huko Taritari, Nueva Esparta, Venezuela Vipindi vya siku Kutwa huko Knysna, Afrika Kusini

UsikuUsiku katiUsiku wa mananeAlfajiriPambazukoAsubuhiAdhuhuriMchanaAlasiriJioniMachweo