Rosemary Karuga

Msanii wa maonesho kenya

Rosemary Namuli Karuga (19 Juni 1928 - 9 Februari 2021) alikuwa msanii wa maonesho kutoka Kenya.[1][2] Mwaka 2017, alitajwa na National Museums of Kenya kuwa Artist of the Month. Alijulikana kama msanii wa kwanza wa kike kusoma katika Chuo Kikuu cha Makerere.[3][4][5][6]

Elimu na miaka ya mwanzo

hariri

Karuga alizaliwa mnamo 1928 huko Meru Kenya. Alisoma katika Chuo Kikuu cha Makerere huko Kampala kati ya miaka ya 1950 na 1952 ambapo alisomea upambaji, upakaji rangi na uchongaji. Mnamo mwaka 2006 alihamia na kuishi na familia yake na kupata matibabu nchini Uingereza.[3][4][5][6] Aliishi huko mpaka kifo chake mnamo 9 Februari 2021.

Baada ya kumaliza elimu yake Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, alirudi Kenya na kufanya kazi ya ualimu.Alistaafu kazi ya ualimu mnamo mwaka 980 na kushawishika na uigizaji. Mnamo 1987, alikuwa mwigizaji wa nyumbani kwenye kituo cha uigizaji cha Paa ya Paa Nairobi. Alitengeneza kituo cha Sanaa kwa kutumia ufungaji wa karatasi kutoka Rexona na sabuni na unga.[2] Mnamo miaka ya 1990 aliagizwa kuonesha kitabu cha Amos Tutuola, The Palm Wine Drinkard. Halafu, maonesho ya chuo chake yalifanyika Paris, Londonna kwenye studio ya makumbusho Harlem, Marekani.[3][4][5][6]

Maisha binafsi

hariri

Aliolewa mnamo mwaka 1953 na kupata watoto watatu na wajukuu.[3][4][5][6]

Marejeo

hariri
  1. "Detail of a collage work by Rosemary Karuga, Untitled, 1998. © Karuga family/Courtesy Red Hill Art Gallery The importance of remembering Kenyan artist Rosemary Karuga". The Conversation. Iliwekwa mnamo 26 Februari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "The Art House - A Profile of Rosemary Karuga - BBC Sounds". www.bbc.co.uk (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2019-12-22.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "Red Hill Art Gallery". www.redhillartgallery.com. Iliwekwa mnamo 2019-12-22.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 "Rosemary Karuga: The masterful artist you've never heard about". Daily Nation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-22.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 "Rosemary Karuga: Unearthing Hidden Artistic Treasures | Contemporary And". www.contemporaryand.com (kwa Kijerumani). Iliwekwa mnamo 2019-12-22.
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 "The nine pioneer women of East African art". The East African (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-22.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rosemary Karuga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.