Ryan Nyambe (alizaliwa 4 Desemba 1997) ni mchezaji wa soka huko Namibia ambaye anacheza kama beki au kiungo wa klabu ya Blackburn Rovers iliyopo nchini Uingereza katika ligi daraja la pili na timu ya taifa ya Namibia.

Kazi ya klabu hariri

Nyambe ambaye anacheza katika klabu ya Blackburn Rovers .Alianza kucheza katika kikosi chake cha kwanza mnamo Agosti 2015 kwenye Kombe la EFL.pia mnamo Julai 2017 alisaini mkataba mpya wa miaka tatu na kilabu hiyo mwisho mwaka 2019 pia Aprili 2019 alisaini mkataba mpya wa miaka mbili na Blackburn Rovers.

Kazi ya kimataifa hariri

Mnamo Mei 2019 Nyambe alisema kuwa alikuwa na "msisimko" kuwakilisha Namibia, nchi yake katika kiwango cha kimataifa.

Alicheza mechi ya kimataifa katika nchi yake ya Namibia dhidi ya Ghana mnamo 9 Juni 2019 huko Dubai.

Mnamo 23 Juni 2019 Nyambe alicheza kwa mara ya kwanza katika mechi waliyofungwa ya Namibia katika raundi ya kwanza ya hatua ya makundi katika kombe la AFCON dhidi ya Moroko. Wakati mechi ilimalizika kwa kufungwa kwa 0-1, Nyambe alipewa sifa ya kucheza vizuri katika mchezo huo.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ryan Nyambe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.