Salama Jabir
Salama Zalhata Jabir (alizaliwa 1 Oktoba 1984) ni mtangazaji wa vipindi vya televisheni kutoka Tanzania[1] — hasa katika televisheni ya Afrika Mashariki (EATV).[2]
Salama Jabir | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | Mtangazaji wa vipindi vya televisheni |
Maisha
haririAlizaliwa kwenye familia ya watoto tisa [3].
Hapo awali, aliolewa na kuachwa,kisha alipata kuwa mtangazaji wa kipindi cha MkasiTv, kilichobuniwa na yeye na A.Y. Kipindi kilikuwa kinarushwa kupitia EATV — ambapo ndani yake wanahoji watu mbalimbali maarufu hadi hapo baadaye walipoamua kukiweka katika idhaa ya YouTube tarehe 1 Novemba 2011[4].
Salama pia ni jaji katika mashindano ya kutafuta vipaji vya wanamuziki yaitwayo Bongo Star Search akionekana kuwa ni jaji asemaye ukweli kwa wanaosailiwa[5].
Mafanikio
haririSalama Jabir amepata mafanikio yafuatayo katika tasnia ya utangazaji na uanzishaji wa vipindi vya televisheni kilichoongeza ubora wa muziki wa Bongo Flava kwa upande wa utayarishaji wa video.
Kabla ya kipindi hiki, wengi hawakuwa wanazingatia ubora wa kazi, lakini kupitia Salama walijitahidi Kuboresha kazi zao kwa upande wa video ili wasije kunangwa naye. Na hivi karibuni amekuWa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kutangaza mpira kwa lugha ya Kiswahili kwenye kituo maarufu cha michezo duniani cha Super Sport [6].
Mtangazaji mwanzilishi wa Mkasi
haririAmefanikiwa kuanzisha na kutangaza katika kipindi cha televisheni cha Mkasi katika televisheni ya EATV.
Baada ya kuacha kurushwa kwa kipindi hiki katika televisheni ya EATV Salama Jabir alianzisha chaneli ya Youtube yenye jina la MkasiTV yenye wateja 123638 mpaka makala hii ilipohaririwa [7].
Mtangazaji wa kipindi cha Shabiki
haririMtangazaji wa kipindi cha televisheni cha Shabiki kinachorushwa katika televisheni ya EATV kinachohusu michezo na mashabiki wakihusishwa na timu baada na kabla ya timuzao kucheza.< [8]
Mtangazaji wa kipindi Ngaz kwa Ngaz
haririSalama pia amefanikiwa kutangaza kipind cha televisheni cha Ngaz kwa Ngaz kinachorushwa na EATV .< [9]
Jaji wa Bongo Star Search
haririSalama Jabir pia amekuwa akishiriki kama jaji katika mashindano ya kuibua vipaji vya wanamuziki yaitwayo Bongo Star Search.
Mwanzilishi wa MkasiTV
haririAmefanikiwa kuanzisha kampuni ya MkasiTV akishirikiana na AY na Josh Murunga[10].
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-30. Iliwekwa mnamo 2018-12-01.
- ↑ https://feisaljumapinto.blogspot.com/2015/06/picha-4-salama-jabir-ndani-ya-mavazi.html
- ↑ https://www.famousbirthdays.com/people/salama-jabir.html
- ↑ https://www.youtube.com/results?search_query=mkasi+tv
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-25. Iliwekwa mnamo 2018-12-01.
- ↑ https://globalpublishers.co.tz/dstv-yamtambulisha-salama-jabir-kutangaza-kiswahili-afcon-2019/
- ↑ https://www.youtube.com/results?search_query=mkasi+tv
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-25. Iliwekwa mnamo 2018-12-01.
- ↑ http://bongo5.com/show-mpya-ya-salama-jabir-ngaz-kwa-ngaz-kuanza-kuruka-leo-eatv-07-2016/
- ↑ http://bongo5.com/show-mpya-ya-salama-jabir-ngaz-kwa-ngaz-kuanza-kuruka-leo-eatv-07-2016/
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Salama Jabir kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |