Sanjaranda ni kata ya Wilaya ya Itigi katika Mkoa wa Singida, Tanzania.

Kata ya Sanjaranda
Nchi Tanzania
Mkoa Singida
Wilaya Wilaya ya Itigi
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 12,560

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 12,560 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,828 waishio humo.[2]

Makabila

hariri

Kata ina vijiji vitatu: Sanjaranda, Gurungu na Kitopeni.

Katika kijiji cha Sanjaranda kuna makabila makuu mawili ambayo ni Wataturu na Wanyaturu. Wenyeji haswa wa kijiji cha Sanjaranda ni Wataturu. Kabila hilo ni jamii ya wafugaji, na ni moja ya makabila ambayo si ya Kibantu na historia inasema ni wahamiaji ambao walitokea Sudani miaka mingi iliyopita.

Kijiji cha Sanjaranda kina mitaa au vitongoji vitano ambavyo ni Utaturuni, Samaria, Pepeani, Majengo na Chang'ombe.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Itigi - Mkoa wa Singida - Tanzania  

Aghondi | Idodyandole | Ipande | Itigi Majengo | Itigi Mjini | Kalangali | Kitaraka | Mgandu | Mitundu | Mwamagembe | Rungwa | Sanjaranda | Tambukareli


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sanjaranda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.