Wanyaturu

Wanyaturu (au Waturu; wao hupendelea kuitwa Arimi, yaani watu wa Rimi [1]) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Singida.

Shujaa wa Kinyaturu

Lugha yao ni Kinyaturu, ambacho ni jamii ya Kibantu, lakini kina fonimu nyingi za Kikushi.

HistoriaEdit

Asili ya kabila hilo inasemekana ni nchi ya Ethiopia ambako kunasadikiwa kuwa na watu wanaotumia lugha ambayo kwa asilimia kubwa inafanana na Kinyaturu. Hudhaniwa pia kuwa Wanyaturu na Wakushi wa Ethiopia asili yao ni moja.

Walipoingia eneo la Tanganyika walichangamana na Wanyatunzu pamoja na Wasukuma, ndiyo maana mila na tamaduni zao zinashabihiana kwa kiasi kikubwa, hivi kwamba ni vigumu kumpambanua Mnyaturu baina ya Wanyatunzu.

Wana utani na Wanyiramba na Wairaqw.

Idadi na mgawanyikoEdit

Mwaka 1993 walikuwa 556,000 [1].

Ndani ya kabila hilo, kuna makundi matatu:

  • Vahi (Wahi), ambao ni zaidi ya nusu ya Wanyaturu wote, na kuwa wenyeji wa mji wa Singida: hao wanaishi kuanzia Singida mjini hadi karibu na wilaya ya Manyoni;
  • Airwana (Wilwana) wanaishi kaskazini kwa ziwa Singida;[2]
  • na lile dogo zaidi la Anyiŋanyi (Wanyinganyi) wanaoishi maeneo ya Mnying'anyi.
  • Unyambwa pia ni sehemu iliyoko Singida na inasemekana ni ukoo mkubwa sana wenye mababu wakubwa wawili: mzee Ghambona na Hante. Ukoo huu hauvumi sana kutokana na watoto wa wazee hao kuhama Unyambwa na kwenda Iguguno, ambako lakini hawakukaa sana, wakahama tena na kuelekea hasa mikoa jirani kama Shinyanga, Tabora na Mwanza. Ni ukoo wenye watoto wengi wa kike kuliko wa kiume, na dini yao kubwa ni Uislamu.

Kuna historia pia ya koo mbalimbali kama Unyanjoka ambao waliongoza sehemu za Wilwana. Ukoo wa Unyanjoka unaanzia Ikhangao na Ndaang'ongo, Ilongero hadi Mtinko na Mpambaa.

TanbihiEdit

  1. Pengine jina "Wanyaturu" linapoteza historia yao kwani liliundwa na Wazungu
  2. Unaweza kubadilisha hapa kuhusu Airwana kuwa si wengi karibu nusu ya Wanyaturu wote kwa ukianzia pale mjini Singida ukielekea Kusini hadi sehemu za Issuna hadi Itigi na Manyoni hadi Kintinku hawa ni Vahi tu, bado sijasema sehemu za Ihanja hadi Muhintiri na sehemu za Mang'onyi na Misughaa ni vahi au wahi kwa hiyo robo tatu ya wanyaturu ni wahi yaani vahi waweza kufanya utafiti na utagundua ukweli huo. wairwana wana maeneo kuelekea Kaskazini ambayo ni sehemu ndogo sana kieneo na inapakana na Wanyiramba ukifika sehemu za Iguguno.
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanyaturu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.