Ol Doinyo Lengai

Mlima wa Mungu
(Elekezwa kutoka Oldoinyo Lengai)

Ol Doinyo Lengai (maana kwa Kimaasai ni "Mlima wa Mungu") ni mlima wenye asili ya volkeno katika Tanzania ya Kaskazini. Iko takriban km 120 kaskazini-magharibi kwa Arusha na km 25 kusini kwa Ziwa Natron.

Ol Doinyo Lengai wakati wa mlipuko wake wa 1966.
Ol Doinyo Lengai kutoka ziwa Natron.

Mlima una kimo cha m 2690 juu ya UB.

Ni volkeno ya pekee duniani kutokana na aina ya lava yake inayotoka hali ya kiowevu (majimaji) lakini si moto sana (mnamo 500° - 600 °C).

Ol Doinyo Lengai ililipuka tena kuanzia Machi 2006. Katika mwaka 2007 mlima umesababisha mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara kuanzia tarehe 12 Julai. Tetemeko la tarehe 18 Julai lilisikika hadi Nairobi.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri