Publius Cornelius Scipio Africanus (236183 KK) [1] alikuwa kiongozi wa kijeshi wa Jamhuri ya Roma na mwanasiasa wakati wa vita ya pili dhidi ya Karthago. Anakumbukwa hasa kwa uongozi wake katika mapambano ya kumshinda Hanibal wa Karthago.

Cornelius Scipio

sanamu ya Scipio Africanus Mzee kwenye Makumbusho ya Pushkin, Moscow.

Muda wa Utawala
205–202 KK, – [?] KK
mtangulizi Quintus Caecilius Metellus na Lucius Veturius Philo
aliyemfuata Marcus Cornelius Cethegus na Publius Sempronius Tuditanus

tarehe ya kuzaliwa 236 KK
Roma, Jamhuri ya Roma
tarehe ya kufa 183 KK (umri 53)
Liternum
ndoa Aemilia Paulla
watoto Publius Cornelius Scipio, Lucius Cornelius Scipio, Cornelia, Cornelia Scipionis Africana
Military service
Nickname(s) Hannibal wa Kiroma
Allegiance Jamhuri ya Roma
Rank Jenerali
Battles/wars Second Punic War
Battle of Ticinus
Battle of the Trebia
Battle of Cannae
Battle of Cartagena
Battle of Baecula
Battle of Ilipa
Battle of Utica
Battle of the Great Plains
Battle of Zama
Roman-Syrian War
Battle of Magnesia

Scipio alishinda mapigano ya Zama katika Afrika ya Kaskazini. Jina lake Africanus (Mwafrika) limetokana na mahali pa ushindi wake, si kutokana na kuzaliwa huko, wala kuwa na ukoo wa Kiafrika. Kutokana na ushindi dhidi ya mpinzani aliyekuwa hatari kuu kwa Roma ya Kale Scipio alikuwa kati ya viongozi wa kijeshi mashuhuri zaidi katika historia ya Dola la Roma. Baada ya mapigano ya Zama Karthago ilipaswa kuomba amani ikapewa masharti ya fedheha.

Marejeo hariri

  1. Alijulikana pia kama Scipio Mwafrika, Scipio Africanus-Major, Scipio Africanus Mzee na Scipio Mkuu.

Vitabu hariri

Maandiko ya Kale hariri

Vitabu vya wataalamu wa kisasa hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: