Sebastian Giovinco


Sebastian Giovinco (alizaliwa mnamo 26 Januari 1987 mjini Turin) ni mwanakandanda mwenye uraia wa Italia anayeichezea klabu ya Serie A ya Juventus. Giovinco ni mchezaji wa kiungo kati anayeshambulia na mwenye ujuzi wa kuchenga na kutengeneza mchezo unaovutia.

Sebastian Giovinco mwaka 2015

Kutokana na kimo na ujuzi wake, Giovinco alipewa jina formica atomica ("mdudu wa kinyuklia", baada ya mhusika wa kipingi cha runinga cha Hanna-Barbera ) na ingawa alikuwa katika hatua za kwanza za wasifu wake wa kandanda, leo anafikiriwa kama mmoja wa wanakandanda wa Kiitaliano wenye ahadi.

Wasifu

hariri

Maisha ya Awali

hariri

Giovinco alizaliwa mjini Turin kwa wavyele wahamiaji wa Italia ya kusini; mama yake anatoka Catanzaro, Calabria na baba yake anatoka Palermo, Sicily. Alilelewa akiwa na hamu sana ya kucheza kandanda na mchezo wake wa kusisimua uliivutia klabu ya Juventus ambao ilimleta katika mfumo wao wa mwaka wa 2001, akiwa na umri wa miaka 14. Kisha akapanda safu za klabu za mfumo wao wa vijana, na alisisimua kwa kushinda Campionato Primavera na bianconeri katika kampeni yao msimu wa 2005-06.

Mchezo wake wa kwanza katika timu ya kwanza ya Juventus

hariri

Giovinco alifaulu kujumuishi katika timu ya Juventus ya kwanza na akacheza mechi yake ya kwanza mnamo 12 Mei 2007 katika ligi ya Serie B dhidi ya Bologna, kuingia kama mbadala wa Raffaele Palladino, na kuashiria mara moja ujuzi wake kwa kumwadalia David Trezeguet pasi safi ambayo aliifunga.

Mkopo katika klabu ya Empoli

hariri

Mnamo 4 Julai 2007 alikopwa nje kwa klabu ya Empoli timu ya Serie A ya Tuscan ambayo pia ilishiriki katika Kombe la UEFA la msimu wa 2007-08. Giovinco alifunga bao lake la kwanza la Serie A mnamo 30 Septemba 2007 wakati Empoli iliicharaza Palermo mabao 3 kwa 1. Bao lake ndilo lililosababisha ushindi.

Giovinco alisababisha riba kutoka kwa vyombo vya habari wakati alifunga bao lake la pili wiki chache baadaye, mnamo 4 Novemba. Bao hilo lilikuwa la kusawazisha katika dakika ya mwisho dhidi ya AS Roma, lilikuwa kombora ndefu lililokunjwa la "free kick" kutoka upande wa kulia, bao ambalo lililinganishwa na baadhi ya wapenda kandanda kama la Ronaldinho dhidi ya Uingereza katika kombe la dunia la mwaka wa 2002.

Kurejea Juventus

hariri

Mnamo 26 Juni 2008 ilithibitisha kuwa Giovinco angerudi Juventus kwa kampeni ya 2008-2009 , kumpatia nafasi ya kucheza katika kiwango cha kombe la mabingwa barani Ulaya vilevile.

Giovinco alicheza mechi yake ya kwanza ya Juventus dhidi ya Catania mnamo 24 Septemba 2008. Giovinco aliingia kama mbadala wa mchezaji mwenzake wa timu ya Juventus,Pavel Nedved, mwisho wa nusu ya pili, na kucheza mchezo wa kusisimua kwa kumwandalia Amauri pasi safi aliofunga katika ushindi wa Juventus wa 1-0. Alifunga bao lake la kwanza katika Jesi ya Juventus dhidi ya wapinzani Lecce tarehe 7 Desemba 2008 kutoka kwa "FreeKick". Giovinco pia amefunga mabao dhidi ya Catania katika Coppa Italia na nyingine dhidi ya Bologna katika maonyesho ya mchezaji bora wa mechi.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Giovinco ameiwakilishwa Italia katika kila kiwango ya vijana kuazia mika chini ya 16 ikiendelia juu. Alitajwa katika kikosi cha Italia ch vijana wasiozidi umri wa miaka 21 na kocha mkuu Pierluigi Casiraghi tarehe 1 Juni 2007 ilikucheza mechi yake ya kwanza katika kiwango hicho katika mechi ya kufuzu dhidi ya Albania. Yeye ndiye aliyemwandalia Acquafresca pasi safi ambaye alifunga. Timu hiyo ya Italia ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ilishinda mechi hiyo 0-1.

Pia alishiriki katika shindano la Toulon mwaka wa {2008 ambapo aliteuliwa kama mchezaji mwenye thamana zaidi au ukipenda mchezaji bora zaidi katika shindano hilo, kwa kufunga mabao mawili katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ivory Coast, na kufunga penalti ya ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Japani. Italia hatimaye ilishinda shindano hilo, kwa kuicharaza Chile 1-0 katika fainali.

Giovinco kisha alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2008 kwa ajili ya timu ya Kiitaliano. Alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Honduras katika mechi ya ufunguzi ya shindano hilo ambapo alifunga bao hilo kutoka nje ya boksi kwa mguu wake wa kushoto. Pia alionyesha mchezo wa kuvutia katika mechi ya pili dhidi ya Korea Kusini. Ndoto yake ya kushinda taji la Olimpiki lilitumbukia nyongo baada ya Italia kupoteza 3-2 dhidi ya Ubelgiji katika robo-fainali.

Juventus:

  • 2005-06 Torneo di Viareggio
  • 2005-06 Campionato Primavera
  • 2006-07 Serie B

Timu ya Kitaifa

hariri

Vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ya Italia

  • 2008 International Tournament of Toulon

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri