Shimbi Kwandele

(Elekezwa kutoka Shimbi Kwendele)

Shimbi Kwendele ni kata ya Wilaya ya Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania yenye msimbo wa posta 25710 [1].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 9,435 [2]. Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa 6,581 [3].

Historia hariri

Kwa kuwa kata ya Shimbi Kwandele iliitwa Shimbi kabla ya kubadilishwa na kugawanywa mwaka 2014 hapa tutazungumzia historia ya kata ya Shimbi kiujumla.

Kunako karne ya 16 na 17 katika nchi ya Wachagga kulikuwa na utawala wake na viongozi wakuu waliitwa Mangi. Katika nchi ya Shimbi nako walikuwa na Mangi wake. Historia ya umangi Shimbi ilianza kwa mzee Makaviha, mwana wa pili wa mzee Kitimbiri, na mjukuu wa mzee M'mamba. Ilikuwa desturi kurithishana umangi, hivyo mzee Makaviha alimrithisha umangi ndugu yake Latemba. Latemba akamwachia umangi mzee Mashaare, Mashaare avivyozeeka akamrithisha umangi mwanae mkubwa Lamasawe, na baadaye Lamasawe akamrithisha umangi mwanae mkubwa Matolo, muda mfupi baadaye Lamasawe aliuliwa kwa vita vya kuvizia "kisooki" ambapo wakati huo Mangi Matolo alikuwa katika nchi ya Usseri karibu na Kenya. Alipopata habari za kuuliwa kwa baba yake alifika Shimbi haraka;  kwa kuwa wauaji walikuwa bado hawajaondoka wakamuua Mangi Matolo wakiwa na nia ovu ya kuuamgamiza utawala wa Shimbi.

Baada ya matukio hayo wananchi wakikubaliana na mwito wa Lamasawe, mzee Mashelle aliyekuwa uhamishoni huko Uruka wa masharti aje awe Mangi Shimbi. Mashelle alikubali na akaiongoza Shimbi kwa mafanikio makubwa. Baada ya mzee Mashelle kuzeeka akamchagua mwanae mkubwa Mzee Leina kuwa Mangi wa Shimbi. Mzee Leina alipoondolewa Umangi, Mzee Mashelle alirudia Umangi Shimbi.

Ilivyokuwa, Mangi Leina alikuwa na makarani wawili, Ali Masharo na Victory Kishindwa ambao walimwibia Mangi Leina shilingi 30 wakala njama na Mangi Selengia wa Mkuu. Hata Mangi Leina alivyoenda kukopa fedha misheni mkuu, Mangi Selengia wa uruka wa mkuu alimshawishi padri asimkopeshe Mangi Leina shilingi 30. Siku ya kukusanya mapato kwa DC wa Moshi fedha ya Mangi Leina ilikuwa pungufu, hivyo akafukuzwa Umangi. Mangi wa uruka wa Usseri Mangi Sengua alipendekeza baba yake Leina mzee Mashelle arudishwe kuwa Mangi wa Shimbi mpaka alipofariki mwaka 1993.

Wasaidizi wa Mangi Mashelle walikuwa:

1. Mashami, mzee Tamira ibara

2. Masho, mzee mwasu, na baadaye marema Moshivira

3. Issia mzee kitara matere

4. Kitirima mzee Manguo mashombo

5. Uua. Mzee ngumia Teng'ute

Shimbi ilitawaliwa na Mangi Selengia wa Mkuu: Baada ya Mangi Mashelle kufariki tarehe 25 Desemba 1923, mwanaye aliyekuwa Mangi, Leina alikwenda Moshi kudai umangi lakini alikataliwa, hivyo Mangi Selengia wa uruka wa mkuu aliambiwa kutawala Shimbi na hivyo Shimbi ukapoteza heshima ya Umangi rasmi mpaka utawala wa kimangi ulipokoma baada ya uhuru. Pamoja na kuwepo kwa wana wengine wa Mzee Mashelle waliokuwa na uwezo wa kutawala kama mzee stameza na Karufu, njama ilifanywa ili kulinganisha uruka wa Shimbi na Mkuu (kirya).

Baada ya Mangi Selengia kupewa utawala wa Shimbi alichagua wasaidizi ambao waliitwa wachili. Alimteua Alli ambaye ndiye aliyelaghai pesa za kodi kwa Mangi Leina hadi kufukuzwa Umangi, Ali alichukiwa na wananchi wa Shimbi kutokana na utawala mbaya.

Katika utawala wake, Alli alihakikisha hapati upinzani kwa watoto na wajukuu wa mzee Mashelle kwa kuwaandikisha kujiunga na jeshi la mkoloni, miongoni mwao ni Cosma (Kashomba) ngalu (Stamesa) William Leina n.k.

Mchili Ali alibadili jina la Shimbi katika uongozi wake na kuiita Mwateni, Ali aliendelea kutawala Shimbi mpaka macho yake yalipokoma kuona tena na baadaye wananchi wa Shimbi walimchagua mzee Baiseli Marenga kiwango ambaye alitawala vizuri na heshima ya Shimbi ilianza kufufuka tena. Kwa sasa Shimbi inatawaliwa na uongozi wa kawaida wa nchi nzima ya Tanzania chini ya maaafisa watendaji wa kata na vijiji.

Tanbihi hariri

  1. "Orodha ya TCRA kuhusu misimbo ya posta ya maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-27. Iliwekwa mnamo 2020-10-15. 
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016, Tanzania Bara, tovuti ya NBS, iliangaliwa Septemba 2020

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Rombo - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania  

Aleni | Chala | Holili | Katangara/Mrere | Kelamfua/Mokala | Kingachi | Kirongo Samanga | Kirwa Keni | Kisale Msaranga | Kitirima | Mahida | Makiidi | Mamsera | Manda | Marangu Kitowo | Mengeni | Mengwe | Motamburu Kitendeni | Mrao Keryo | Nanjara | Ngoyoni | Olele | Reha | Shimbi | Shimbi Kwandele | Tarakea Motamburu | Ubetu Kahe | Ushiri Ikuini

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Shimbi Kwandele kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.