Shirika la Harakati za Skauti Duniani

Shirika la kimataifa la hesabu

Shirika la Harakati za Skauti Duniani (kwa Kiingereza: World Organization of the Scout Movement - WOSM) ni shirika la skauti duniani ambalo kwa sasa linaunganisha zaidi ya maskauti milioni 57 [1] katika nchi 173. Pia lina kiti katika Kamati ya Kimataifa ya ISGF/AISG (Ushirika wa Kimataifa wa Skauti), ambalo ni shrika la skauti wazee.

Nembo ya Shirika la Harakati za Skauti Duniani.

WOSM iliibuka kutoka Boy Scouts International Bureau iliyoanzishwa mwaka wa 1920.

Nembo ya WOSM ni alama ya yungiyungi ya kifedha kwenye mandharinyuma ya zambarau ishara ya pamoja ya skauti wote wanaoshirikiana katika shirika hilo. Kamba yenye fundo la mfumaji inayozunguka yungiyungi inaashiria mshikamano wa maskauti wote duniani.

Tanbihi

hariri
  1. WOSM: https://www.scout.org/, abgerufen am 22. Dezember 2022

Viungo vya nje

hariri