Sidi Touré
Sidi Touré (alizaliwa 1959, Gao, Mali) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Bamako, Mali . Muziki wake ni aina ya nyimbo ya songhaï blues. Alianza kazi yake katika bendi ya Sonhaï Stars mnamo 1984 alishinda tuzo ya mwimbaji bora katika Mali National Biennale. Alishinda tena tuzo hiyo hiyo mnamo 1986. Mnamo 1992 alishirikiana na Kassemady Diabate.
Nje ya Mali, Sidi Touré anajulikana sana kwa kuonekana kwake katika mfululizo wa video za Take-Away Show ya Vincent Moon. Moon alimrekodi mwanamuziki huyo wa Mali akiwa eneo la kushutia nchini Mali.
Orodha ya kazi za muziki
hariri- Hoga, 1996, Stern's Records
- Sahel Folk, 2011, Thrill Jockey Records
- Koima, 2012, Thrill Jockey Records
- Alafia, 2013
- Toubalbero, 2018
- Afrik Toun Mé, 2020, Thrill Jockey Records
Viungo vya nje
hariri- Sidi Touré on Myspace (official website)
- Sidi Touré Archived 28 Septemba 2010 at the Wayback Machine. in the Take-Away Show
- HOGA Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine. at Sterns Records
Marejeo
hariri- Bio Archived 28 Februari 2020 at the Wayback Machine. on The African Music Guide by Frank Bessem