Sikukuu

(Elekezwa kutoka Siku kuu)

Sikukuu ni siku maalumu ya kukumbuka, kusheherekea au kufurahia jambo fulani.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakifanya Swala ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr,nchini Somalia

Kuna sikukuu za binafsi na sikuu za umma. Sikukuu ya umma mara nyingi huwekwa wakfu kisheria maana yake si siku ya kazi bali ya mapumziko.

Kati ya sikuu za umma kuna sikukuu za kidini na sikukuu za kiserikali.

Kati ya sikukuu za binafsi kuna siku za kukumbuka matukio ya pekee kama tarehe ya kuzaliwa, kumbukumbu ya siku ya kufunga ndoa na mengine.

Sikukuu za kidini

hariri

Sikukuu za Ukristo

hariri

Sikukuu za Uislamu

hariri

Sikukuu za Kiislamu hufuata kalenda ya Kiislamu. Kwa hiyo tarehe za sikukuu hizi katika kalenda ya Gregori hubadilikabadilika.

Sikukuu za Uhindu

hariri
  • Diwali pia "Deepavali" - mwezi wa Oktoba au Novemba

Sikukuu za Serikali

hariri

Hutofautiana kati ya nchi na nchi lakini mara nyingi huwa na: