Simeon Mulama
Simeon Mulama (alizaliwa mnamo 6 Agosti 1980 katika eneo la Huruma, katika mji mkuu wa Nairobi) ni mwanakandanda wa kitaifa wa Kenya aliyestaafu mwaka wa 2009.
Senior career* | |||
---|---|---|---|
Miaka | Timu | Apps† | (Gls)† |
1997 | Mathare United | ||
1998 | AFC Leopards | ||
1999–2001 | Mathare United | ||
2001–2002 | Ismaily | ||
2002–2005 | Park University | ||
2007 | Skellefteå FF | ||
2009– | Mathare United | ||
Timu ya Taifa ya Kandanda | |||
2000–2001 | Kenya | 11 | (1) |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 3 August 2011. † Appearances (Goals). |
Wasifu
haririMulama alianza kucheza akiwa katika Shule ya Msingi ya Dr Aggrey. Kisha alijiunga na Shule ya Upili ya Kakamega na baadaye Shule ya Upili ya Kisii. Mwaka wa 1996 aliichezea timu ya ligi ya mkoa ya Gusii Mwalimu. Alihamia timu ya Ligi ya Kuu ya Kenya ya Shabana Kisii. Mwaka wa 1998 alihamia timu ya AFC Leopards na walishinda taji la ligi mwaka huo. Kisha alihamia Mathare United na baadaye alihamia klabu za Al-Ismaily, Chuo Kikuu cha Park na kisha akapata fursa kwenda katika nchi ya Uswidi kuichezea klabu ya Skellefteå FF.
Mulama alianza kozi ya ukufunzi katika udhamini wa soka nchini Marekani akiwa katika Chuo Kikuu cha Missouri na mwaka wa 2008 alikuwa Mkufunzi mkuu wa klabu ya AC Nakuru.
Hata hivyo, alirejea uwanjani mwaka wa 2009 na aliichezea klabu yake ya zamani ya Mathare United.
Binafsi
haririSimeoni ni pacha wa mchezaji mwenzake Titus Mulama.
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Profile on National-Football-Teams.com
- Mahojiano na Simeon Mulama Ilihifadhiwa 7 Januari 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu Mchezaji Soka wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Simeon Mulama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |