Sint Maarten (yaani Mtakatifu Martino) ni nchi ya visiwani katika bahari ya Karibi (Amerika ya Kati). Iko kwenye sehemu ya kusini ya kisiwa cha Saint Martin kilichogawiwa baina ya Ufaransa na Uholanzi.

Ramani inayoonyesha pande mbili za kisiwa: ule wa Kifaransa Saint-Martin (kaskazini) na ule wa Kiholanzi Sint Maarten (kusini).

Sint Maarten ilikuwa koloni la Uholanzi; sasa ni "nchi ya kujitawala" ndani ya muundo wa "Ufalme wa Nchi za Chini" pamoja na Uholanzi yenyewe na nchi nyingine zilizokuwa makoloni ya Uholanzi.

Katika eneo la kilometa mraba 37 wanaishi watu 40,120.

Lugha ya wengi (asilimia 67) ni Kiingereza, ikifuatwa na Kihispania.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti (karibu asilimia 50) halafu Wakatoliki (asilimia 33).

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Miundo mingine
Vyuo vikuu
Elimu ya sekondari
Utalii
Habari na rai
  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sint Maarten kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.