Siri (kutoka neno la Kiarabu) ni jambo lolote ambalo mtu analiona haifai kumshirikisha mtu yeyote yule, haijalishi ni nani.

Pengine siri ni suala la uhai au kifo, kama wakati wa Vita vikuu vya pili.

Kila mmoja ana haki ya kuwa na siri zake.

Katika maisha ya jamii, siri ni muhimu, kiasi kwamba ni wajibu kwa baadhi ya kazi, kama vile ushauri, uganga, huduma za benki n.k.

Siri kali zaidi, katika Kanisa Katoliki, ni ile ya padri kuhusu maungamo aliyopokea katika sakramenti ya kitubio.

Watu wa nadharia za njama mara nyingi huona siri nyuma ya mambo mengi. Kwa mfano, mwaka 2015, taarifa katika gazeti kuhusu ugunduzi wa simu ya mkononi ya miaka 800 huko Austria iliwavuruga wengine kwa muda.[1]

Iligundulika kuwa kipande cha sanaa kilichoitwa Babylonokia Watu wa nadharia za njama walichukulia picha yake kama ugunduzi wa kisayansi na kuieneza mitandao ya kijamii, ikageuka kuwa ni jambo maarufu kwenye mtandao.

Marejeleo

hariri
  1. Evon, Dan (4 Januari 2016). "FALSE: 800-Year-Old Alien Cellphone Found". snopes. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)