Smoke Two Joints
"Smoke Two Joints" ni wimbo ulioandikwa awali na "The Toyes", ambao waliuimba kwa mtindo wa Reggae na kuutoa mwaka wa 1983. Kulingana na "The Toyes", "siku moja tulivu na nzuri iliangukia kwenye kisiwa kidogo cha Oahu huko Hawaii, washiriki wawili wa bendi hio, Mawg na Sky, walikuwa wameketi chini ya mti mkubwa wa banyan kwenye ufukwe wa Kuhio,[1] wakivuta bangi" ndipo ambapo walikuja na wazo la nyimbo hii "Smoke Two Joints."
Nyimbo hii ilitumika kwenye wimbo wa filamu ya kuchekesha ya Marekani ya 1998 iitwayo Homegrown.[2] Toleo la "The Toyes" lilionyeshwa katika mchezo wa video wa 2005 NARC. Wimbo huu mara nyingi unahusishwa kimakosa na Bob Marley kwenye mitandao na tovuti za kijamii. Marley alikuwa ameshafariki miaka miwili wakati wimbo huu ukiandikwa.
Toleo la Nardini
haririNorman Nardini, aliyeko Pittsburgh, Pennsylvania, aliunda matoleo mawili au zaidi ya wimbo huu katika miaka ya 1980. Moja ilikuwa toleo la studio ya LP, na nyingine ilikuwa toleo lililoangaziwa kwenye kanda yake ya moja kwa moja kutoka 1994, zote zilitayarishwa na lebo ya muziki ya "Circumstantial Records", iliyoko jiji la New York. Norman alipata wimbo huo kwa mara ya kwanza mwaka wa 1983 wakati rafiki yake Stush alipoleta rekodi ya nyimbo 45 nyumbani kama sehemu ya muziki aliokuwa ameununua wakati wa likizo huko Hawaii. Nardini alikuwa na bendi yake kujifunza,na amekuwa akiimba wimbo huo kwa zaidi ya miaka ishirini. Alitaka kupeperusha toleo la wimbo huo kwenye CBS katika miaka ya 1980, lakini lebo hiyo haikuweza kufuatilia waandishi asilia wa wimbo huo.[onesha uthibitisho]
Toleo la bendi ya Sublime
haririBendi ya Sublime ilitoa toleo la wimbo huu kwenye albamu yao ya kwanza 1992 iitwayo 40oz. to Freedom. " "Smoke Two Joints"" ilikuwa miongoni mwa nyimbo za kwanza kuchezwa kwenye redio[onesha uthibitisho] baada ya nyimbo ya "Date Rape". Toleo hili linajumuisha vipande vya muziki vilizochukuliwa kutoka kwenye filamu ya Beyond the Valley of the Dolls [3] (ingawa utangulizi huu kwa kawaida huondolewa wakati wimbo ukichezwa kwenye redio), na kwa wasanii Eazy-E na Just Ice. Bert Susanka, mwimbaji mkuu wa "The Ziggens" (mshawishi mkubwa kwa Sublime), pia ametolea msemo akisema akisema, "Smoked cigarettes 'til the day she died!" Wimbo huo pia umeangaziwa kwenye filamu ya Saga ya mwaka wa 2003 na iko kwenye wimbo wa Saga kama toleo fupi zaidi. Wimbo huo pia unatumika katika filamu ya Mallrats wakati washiriki wa onyesho la mchezo kupewa bangi na Jay na Silent Bob.
"Smoke Two Joints" iliachiwa rasmi 1994.
Toleo la Sublime limekuwa likitumika katika mchezo wa video wa Rocksmith 2014.
Matoleo Mengine
hariri- Richard Cheese hutumbuiza wimbo huu kwenye albamu yake ya Tuxicity.
- Kundi la ska punk "The Rudiments" hutumbuiza toleo la wimbo huu kwenye albamu yao ya Psychoska ambalo linatanguliwa na video fupi kutoka kwa Cheech na Chong la sinema.
- Bendi ya Ujerumani "Ohrbooten" iliuimba kwa Kijerumani.
- Rapa wa kijerumani Timi Hendrix aliuimba kwa kijerumani.
- South Park Mexican wameunda toleo la wimbo huu ambalo linaweza kupatikana kwenye albamu yao yaThe Purity Album.
- Afroman aliufanya wimbo huu kwa namna ya uiimbaji wa majibizano ukiitwa "Smoke 2 Blunts"
- Macy Gray aliachia toleo la wimbo huu katika albamu yake ya 2012 iitwayo Covered.[4][5]
- "Insanity Alert" ilitoa toleo la wimbo huu kwenye albamu yao ya 2019 "666-Pack". Ulikuwa ni Wimbo wa 13 ukiitwa "Two Joints".
Marejeo
hariri- ↑ "Smoke Two Joints". www.thetoyes.com. 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Februari 2011. Iliwekwa mnamo 15 Machi 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The SoundtrackInfoProject: Homegrown (1998)".
- ↑ Grim, Ryan (2009). This Is Your Country on Drugs: The Secret History of Getting High in America'. John Wiley & Sons, Inc. uk. 99.
- ↑ Partridge, Kenneth. "Macy Gray 'Smoke Two Joints' Video: Singer Throws Reggae Dance Party". AOL. Iliwekwa mnamo 2 Aprili 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Video katika YouTube