Nation Media Group
Nation Media Group (NMG) ni kundi la vyombo vya habari vya Kenya lililoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi.[1]
NMG ilianzishwa mwaka wa 1959 na ndilo shirika kubwa la binafsi la vyombo vya habari katika Afrika Mashariki na Kati na lina ofisi nchini Kenya, Uganda na Tanzania.[2]
Mwaka wa 1999, NMG ilianzisha NTV, kituo cha habari nchini Uganda, na Easy FM.[3]
Tangu 2001 NMG imemiliki kampuni ya habari ya Tanzania inayoitwa Mwananchi Communications Ltd. yenye kutoa magazeti kama vile Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen.
Katika Kenya na Uganda NMG inachapisha The EastAfrican, Daily Nation (gazeti kuu nchini Kenya), The Business Daily, Daily Monitor, NMG Investor Briefing , Taifa Leo na Zuqka.
Tanbihi
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-25. Iliwekwa mnamo 2009-12-25.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-11. Iliwekwa mnamo 2009-12-25.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-11. Iliwekwa mnamo 2009-12-25.