Korobindo (Ploceidae)
(Elekezwa kutoka Sporopipes)
Korobindo | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Korobindo paji-madoa (Sporopipes frotalis
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 5, spishi 10:
|
Korobindo ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Ploceidae. Kuna ndege wengine ambao wanaitwa korobindo katika familia Passeridae. Spishi hizi zinatokea Afrika tu.
Ndege hawa wanafanana na shomoro lakini wana mwenendo kama kwera. Wana rangi ya kahawa au kijivu juu na nyeupe chini. Hula mbegu hasa na beri na wadudu pia.
Spishi hizi hulijenga tago lao ndani ya msongo wa manyasi na pengine vijitu pia ambao umebandikiwa tawi la mti. Korobindo mpendakundi hujenga jengo kubwa la manyasi linaloweza kuwa na nafasi kwa matago zaidi ya 100. Majengo haya yapo katika miti au juu ya nguzo zilizowekwa na watu kama vile nguzo za umeme. Jike huyataga mayai 3-5.
Spishi
hariri- Histurgops ruficauda, Korobindo Mkia-mwekundu (Rufous-tailed Weaver)
- Philetairus socius, Korobindo Mpendakundi (Sociable Weaver)
- Plocepasser donaldsoni, Korobindo wa Donaldson (Donaldson-Smith's Sparrow Weaver)
- Plocepasser mahali, Korobindo Nyusi-nyeupe (White-browed Sparrow Weaver)
- Plocepasser rufoscapulatus, Korobindo Mgongo-mwekundu (Chestnut-backed au Rufous-mantled Sparrow Weaver)
- Plocepasser superciliosus, Korobindo Utosi-mwekundu ( Chestnut-crowned Sparrow Weaver)
- Pseudonigrita arnaudi, Korobindo Utosi-kijivu (Grey-capped au Grey-headed Social Weaver)
- Pseudonigrita cabanisi, Korobindo Utosi-mweusi (Black-capped Social Weaver)
- Sporopipes frontalis, Korobindo Paji-madoa (Speckle-fronted Weaver)
- Sporopipes squamifrons, Korobindo Masharubu (Scaly-fronted Weaver)
Picha
hariri-
Korobindo mkia-mwekundu
-
Korobindo mpendakundi
-
Korobindo wa Donaldson
-
Korobindo nyusi-nyeupe
-
Korobindo mgongo-mwekundu
-
Korobindo utosi-mwekundu
-
Korobindo utosi-kijivu
-
Korobindo utosi-mweusi
-
Korobindo masharubu