Stadi za lugha ni zile mbinu ambazo mkufunzi anazitumia kufundisha lugha asilia kwa msomi wa lugha ya pili. Pia ni mbinu msomi wa lugha ya pili anazotumia kuhakikisha amempata mkufunzi wa lugha ya pili kiufasaha.

Stadi hizo pia zinaweza kuitwa mbinu za ufundishaji wa lugha ambazo nazo ni kama vile: kusikiliza na kuongea, kusoma, kuandika sarufi katika lugha funzwa na msamiati wa lugha funzwa.

Ni lazima mfundishaji wa lugha afuatilie utaratibu fulani ili aweze kuhakikisha wanafunzi wake wanampata ipasavyo. Mwalimu hawezi kufunza mwanafunzi kuandika kama hana ufahamu wa kusoma. Kwa hiyo, ni lazima afundishe mwanafunzi kusoma kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kumfundisha jinsi ya kuandika.

Maana yake

hariri

Lugha ni kipengele muhimu sana katika mwasiliano na husaidia na kuwezesha watu kutagusana ama kutangamana. Kuna stadi nne za msingi ambazo huwezesha watu kubadilishana mawazo, fikra na hisia. Kuzifahamu vyema stadi hizo, au tuseme kuzidhibiti, kunatusaidia kuwasiliana na wengine katika shughuli zetu za kila siku kwa mafanikio tunayotarajia. Stadi hizo za lugha ni nne:

  1. Kusikiliza
  2. Kuzungumza
  3. Kusoma
  4. Kuandika

Tunapojifunza lugha, tunahitaji kudhibiti stadi hizi nne muhimu ili tuweze kuwasiliana kwa njia mwafaka. Kati ya stadi hizo, mbili, yaani kusikiliza na kusoma, ni za kupokea yaani stadi pokezi, ilhali kuzungumza na kuandika ni za kutoa ama stadi elezi.

Tunapojifunza lugha mama au lugha ya kwanza, tunaanza kwa kujifunza kusikiliza, halafu tunajifunza kuzungumza. Kisha tunajifunza kusoma na mwisho, kuandika.

Ikumbukwe kwamba stadi hiziohuhusiana na kutegemeana, yaani zinajengana. Kwa mfano, bila kusikiliza huwezi kukuza stadi ya kuzungumza. Hali kadhalika stadi ya kuandika hujengwa na kuimarishwa na kusoma.

Uwezo wa kutumia lugha katika mawasiliano hautokani na stadi mmoja bali na stadi zote nne za lugha. Kwa hiyo kabla ya kuzungumzia mbinu za kufundisha stadi za lugha, ni muhimu sana kufahamu stadi hizo zikoje.

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stadi za lugha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.