Tadrart Rouge (yaani "Mlima Mwekundu" pia: Southern Tadrart, Algerian Tadrart au Meridional Tadrart) ni safu ya milima kusini mashariki mwa Algeria, sehemu ya jangwa. Huko inapatikana michoro ya miambani kwa wingi.

Hali ya hewa

hariri

Tadrart Rouge kwa sasa kuna jua kali na ni pakavu bila mvua kabisa. Lakini wakati wa unyevu wa Kiafrika eneo hilo lilikuwa na mvua na lilifunikwa na mimea ya savanna, hivyo lilikuwa linafaa kwa maisha ya binadamu na wanyama. [1]

Sanaa za kwenye miamba

hariri

Tadrart Rouge ina sanaa nzuri ya miamba ya Sahara inayofunika urefu wa muda kutoka kipindi cha Neolithic hadi nyakati za hivi karibuni. Kuta za miamba na makao ya miamba kwenye wadi zimejaa michoro ya miamba na michoro hiyo imeandikwa mabadiliko ya hali ya hewa wakati eneo hilo lilibadilika kutoka savanna miaka 10,000 iliyopita hadi kuwa jangwa miaka 5,000 iliyopita. Sanaa ya miamba ilibadilika kwa wakati kutoka kwa wanyama pori kama Tembo, Faru, Twiga, Swala, na Jamii ya bovidae mwitu, kuwa wanyama wa kufugwa kama bovids, ovicaprids, Farasi, na Ngamia.

Marejeo

hariri
  1. Stefan Kröpelin et al., Climate driven ecosystem succession in the Sahara: The past 6000 years. Science 2008, 320, pp. 765–768.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tadrart Rouge kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.