Taiga (kwa Kiingereza[1] pia boreal forest [2] au snow forest [3]) ni jina la maeneo makubwa ya misitu kaskazini mwa dunia inayofanywa na aina mbalimbali ya miti ya misunobari, katika Eurasia pia pamoja na mibetula. Takriban 29% za misitu yote duniani ni aina ya taiga.

Uenezaji wa taiga duniani, inapatikana katika kaskazini kama kanda pana kati ya taiga na mbuga baridi.
Misonobari kwenye taiga ya Alaska.

Taiga inafunika sehemu kubwa za Alaska, Kanada, Uswidi, Ufini, Norwei, Kazakhstan ya kaskazini na Urusi (hasa Siberia) pamoja sehemu nyingine za kaskazini za Marekani.

Maeneo ya taiga yako upande wa kusini wa kanda la tundra. Katika Urusi taiga inafuatwa na kanda la mbuga baridi kusini mwake.

Kwa jumla tabianchi kwenye taiga ni baridi sana kwa miezi mingi ya mwaka[4]. Majirajoto ni fupi, kwa kawaida miezi 1-2 pekee. Taiga ya Siberia wastani ya halijoto wakati wa baridi ni kati ya -6°C na -50°C.[5]

Marejeo hariri

  1. Asili ya jina iko katika lugha za Kiturki
  2. msitu wa kaskazini
  3. msitu wa theluji
  4. radford:Taiga climate. Radford.edu. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-06-09. Iliwekwa mnamo 2011-02-21.
  5. Encyclopedia Universalis édition 1976 VOL.2 ASIE – Géographie physique, page 568 (Kifaransa)

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: