Jangwa la Taklamakan

(Elekezwa kutoka Taklamakan Desert)

Jangwa la Taklamakan (pia: Taklimakan na Teklimakan) ni jangwa kaskazini magharibi mwa China. Ni sehemu katika kusini magharibi mwa Mkoa wa Xinjiang. Upande wa kusini iko Milima ya Kunlun, upande wa magharibi na kaskazini Milima ya Pamir na milima ya Tian Shan.

Jangwa la Taklamakan.
Ramani ya Taklamakan.

Oasisi

hariri

Ni eneo yabisi sana na zamani wasafiri waliofuata Barabara ya Hariri walipaswa kuvuka jangwa hilo wakitumia miji ya oasisi kwenye kusini au kaskazini ya jangwa iliyotumia maji chini ya ardhi yaliyoshuka kutoka milima. [1] Miji muhimu ya oasisi ilikuwa Kashgar, Marin, Niya, Yarkand, na Khotan upande wa kusini, Kuqa na Turpan kaskazini, na Loulan na Dunhuang mashariki. [2] Siku hizi wakazi wa miji hii ni hasa Wauiguri.

Tabianchi

hariri

Milima ya Himalaya inazuia mvua kutoka bahari kufika eneo la Taklamakan na hivyo kusababisha ukame wake. Hewa baridi kutoka Siberia upande wa kaskazini inaweza kufika, kwa hiyo sentigredi °C -40 zimeshapimwa kwenye majira ya baridi, lakini majira ya joto sentigredi za °C +40 zinawezekana pia.

Mwaka 2008 Taklamakan yote ilifunikwa na tabaka la theluji.[3]

Marejeo

hariri
  1. Spies Along the Silk Road. Iliwekwa mnamo 2007-08-07.
  2. "The Silk Road". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-15. Iliwekwa mnamo 2007-08-07.
  3. "China's biggest desert Taklamakan experiences record snow", Xinhuanet.com, February 1, 2008. 
  Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jangwa la Taklamakan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.