Tanzanaiti (kwa Kiingereza: Tanzanite) ni kito chenye rangi ya buluu hadi zambarau na kijani. Inachimbwa kaskazini mwa Tanzania tu.

Kito cha Tanzanaiti katika hali asilia
Tanzanaiti baada ya kukatwa na kung'arishwa

Kito hicho kinapendwa sana kimataifa; bei zake zilicheza kati ya dola za Marekani 250 na 500 kwa karati moja (=milligramu 200).

Kikemia ni aina ya madini ya Zoiziti ambayo haina thamani kubwa vile katika maumbo mengine. Lakini tanzanaiti bandia inatengenezwa kwa kupasha moto fuwele za zoiziti ya kawaida zinazobadilika rangi motoni.

Tanzanaiti iligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1967 katika milima ya Mererani kwenye Wilaya ya Simanjiro, karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na mji wa Arusha. Iligunduliwa na Mtanzania aitwaye Jumanne Mhero Ngoma mkoani Manyara. Manuel D'souza alituma sampuli hiyo kwa mwanajiolojia John Saul ambaye ana cheo cha PhD kutoka chuo cha M.I.T., ambaye alituma sampuli hiyo kwa baba yake, ikapelekwa Havard University kwa wataalamu wa madini na kuthibitishwa kwamba ilikuwa ni kito cha Aina ya Zoizite.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tanzanaiti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.