Teknolojia ya habari

(Elekezwa kutoka Teknolojia ya Habari)

Teknolojia ya habari na mawasiliano (kifupi: TEHAMA; kwa Kiingereza: information technology, kifupi: IT), kama ilivyoainiwa na Shirikisho la Teknolojia ya Habari ya Marekani (ITAA), ni "utafiti, urasimu, uendeleshaji, utekelezaji, usaidizi au usimamizi wa mifumo ya habari, hasa ala za programu na vifaa vya kompyuta." [1].

Taarifa ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika mwaka wa 2005

TEHAMA inahusika na matumizi ya kompyuta na programu za kompyuta: kubadili, kuhifadhi, kulinda, kuchecheta, kueneza na usalama katika kupokea habari.

Leo, neno habari limezunguka nyanja nyingi za kompyuta na teknolojia na limekuwa maarufu sana. Wataalamu wa TEHAMA hutekeleza majukumu mbalimbali kutoka kuweka ala hadi kubuni mitandao tata ya kompyuta na hifadhidata. Machache kati ya majukumu ya wataalamu wa TEHAMA ni kufanya usimamizi wa data, kujumuisha kompyuta ili kutengeneza mtandao, uhandisi wa hifadhidata na programu na vilevile usimamizi na utawala wa mfumo mzima.

Wakati kompyuta na teknolojia za mawasiliano zinapounganishwa, matokeo ni teknolojia ya habari ("infotech"). Teknolojia ya habari ni neno la jumla linaloelezea teknolojia yoyote ambayo husaidia katika kuzalisha, kuendesha, kuhifadhi, kuwasilisha, na / au kusambaza habari. Kwa makadirio, wakati tunapozungumza kuhusu teknolojia ya habari kwa ujumla, ni bainisho kuwa matumizi ya kompyuta na habari yanashirikiana.

Katika siku za majuzi ABET na ACM zimeshirikiana kuunda kanuni za akredishon na mitaala Ilihifadhiwa 16 Machi 2010 kwenye Wayback Machine. ya shahada katika teknolojia ya habari kama uwanja wa masomo uliotofautiana na Sayansi ya kompyuta na pia mifumo ya habari. SIGITE ni kikundi cha kazi cha ACM kilichopewa jukumu la kuweka kanuni hizi.

Marejeo

hariri
  1. ITAA.org Ilihifadhiwa 4 Machi 2009 kwenye Wayback Machine., p30, Iliangaliwa 3 Machi 2008

Kwa masomo zaidi

hariri
  • The Global Information Technology Report 2008–2009 (PDF). World Economic Forum and INSEAD. 2009. uk. 406. ISBN 978-92-95044-19-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2009-10-01. Iliwekwa mnamo 2009-12-01.
  • Adelman, C. (2000). A Postsecondary Universe: The Certification System in Information Technology. Washington, DC: US Department of Education.
  • Allen, T., na MS Morton, eds. 1994. Information Technology and the Corporation of the 1990s. New York: Oxford University Press.
  • Shelly, Gary, Cashman, Thomas, Vermaat, Misty, na Walker, Tim. (1999). Discovering Computers 2000: Concepts for a Connected World... Cambridge, Massachusetts: Course Technology.
  • Webster, Frank, na Robins, Kevin. (1986). Information Technology-A Luddite Analysis. Norwood, NJ: Ablex.

Viungo vya nje

hariri