Lango:Afrika
Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.
Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile. Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua). ![]() Robert Gabriel Mugabe (* 21 Februari 1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi. Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashataka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola.
......kwamba Hifadhi ya Arusha inapatikana katika mji wa Arusha nchini Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 542, iko umbali wa kilometa 32 kutoka katika mji wa kitalii wa Arusha.
|