Ngisi

(Elekezwa kutoka Teuthida)
Ngisi
Ngisi mapezi-makubwa (Sepioteuthis lessoniana)
Ngisi mapezi-makubwa (Sepioteuthis lessoniana)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Mollusca (Wanyama bila mifupa wenye ulimi kama tupa)
Ngeli: Cephalopoda
Oda ya juu: Decapodiformes
Oda: Teuthida
Ngazi za chini

Nusuoda 2:

Ngisi ni wanyama wa bahari wenye minyiri kumi. Minane baina ya hiyo huitwa mikono na miwili mingine ni minyiri kweli. Kwa urefu wote wa chini ya mikono kuna vikombe vya kumung'unyia vilivyo na vikulabu mara nyingi. Minyiri inabeba vikombe kama hivi juu ya bako mwishoni.

Minyiri hutumika kwa kukamata wanyama wadogo na mikono hutumika kwa kushika mawindo wakati mnyama akiyakula. Ngisi wana domo linalofanana na lile la kasuku ili kupapua nyama kutoka mawindo.

Ngisi huogelea kwa kuondoa maji kwa nguvu kupitia mrija (siphon) wao. Wanaweza kubadilisha rangi yao na kufanana na kinyume ili kujificha kwa mawindo na maadui. Wakivumbuliwa na adui huruka wakitoa ghubari la kiwi (maada kama wino) ili kumkanganya.

Ukubwa wa takriban spishi zote ni chini ya sm 60 lakini ngisi mkubwa inaweza kufika m 13 na ngisi dubwana inafika hata m 14. Ngisi dubwana mkubwa kuliko wote waliokamatwa alivuliwa mwaka 2007 karibu na Antakitiki. Uzito wake ulikuwa kg 495 na urefu wake m 10.

Kama chakula

hariri

Ngisi huliwa sana na watu duniani kote. Chakula hiki huitwa kalamari.

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngisi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.