Kasuku
Kasuku Mkia-mwekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Psittaciformes (Ndege kama kasuku)
Familia: Psittacidae (Ndege walio na mnasaba na kasuku)
Nusufamilia: Psittacinae (Ndege walio na mnasaba na kasuku)
Jenasi: Jenasi za Afrika:

Agapornis Selby, 1836
Coracopsis Wagler, 1832
Lophopsittacus Newton, 1875
Mascarinus Lesson, 1830
Necropsittacus Milne-Edwards, 1873
Poicephalus Swainson, 1837
Psittacula G. Cuvier, 1800
Psittacus Linnaeus, 1758

Spishi: Angalia katiba

Kasuku ni ndege wa familia Psittacidae. Spishi za jenasi nyingine zinaitwa kwao au cherero. Kasuku wengine ni wakubwa, wengine wadogo. Wengi wana rangi kali. Wana mkia mrefu na miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Domo lao lina nguvu sana na mataya yamepindika kwa pande za kuelekea kama koleo. Kasuku wanatokea kanda zote za tropiki za dunia. Hula mbegu, kokwa, tunda na macho ya maua, pengine wadudu na wanyama wadogo pia. Spishi za “lories” na “lorikeets” hula mbochi na matunda mororo. Kasuku takriban wote hutaga mayai yao tunduni kwa mti.

Spishi ya AfrikaEdit

Jenasi za mabara mengineEdit

PichaEdit