Thaura (kutoka neno la Kiarabu) ni aina ya mapinduzi ambapo serikali hugeuzwa na jeshi au watu wanaohusiana na serikali bila wananchi kwa jumla kushiriki. 

Aina hariri

  • Thaura iliyoshindikana au jaribio la mapinduzi.
  • Thaura isiyo na mabadiliko ya utawala. Kwa mfano kiongozi akitolewa madarakani bila kubadilisha kikundi cha watawala.
  • Ubadilishaji wa dikteta aliyeko kwa mwingine.
  • Kupindua udikteta na kufuatilia na demokrasia[1]

Majibu ya kimataifa hariri

Mashirika kama vile Umoja wa Afrika na Ushirika wa Nchi za Amerika yamepitisha mifumo ya kupambana na mapinduzi ya kijeshi. Kupitia tishio la vikwazo, mashirika hayo hujaribu kukabiliana na mapinduzi ya kijeshi. Utafiti wa mwaka 2016 umegundua kuwa Umoja wa Afrika unachukua hatua za maana katika kupunguza thaura katika bara la Afrika.[2]

Marejeo hariri

  1. Varol, Ozan O. (7 November 2017). The Democratic Coup d'État. Oxford University Press.
  2. Powell, Jonathan; Lasley, Trace; Schiel, Rebecca (7 January 2016). "Combating Coups d’état in Africa, 1950–2014" (in en). Studies in Comparative International Development: 1–21. doi:10.1007/s12116-015-9210-6 . ISSN 0039-3606 . https://link.springer.com/article/10.1007/s12116-015-9210-6.