The Wiz ni tamthiliya na baadaye filamu ya muziki kutoka nchini Marekani. Muziki ilitungwa na Charlie Smalls, kitabu chake na William F. Brown. Ilionyeshwa mara ya kwanza kwenye jukwaa ya Majestic Theatre kwenye Broadway mjini New York, maonyesho ya kwanza yalitokea 5 Januari mwaka 1975.

Picha ya rekodi ya nyimbo za igizo ya The Wiz

Igizo hili linasimulia upya riwaya mashuhuri ya watoto "The Wonderful Wizard of Oz" ikwekwa katika mazigira ya utamaduni ya Wamarekani weusi wa kisasa. Jina la igizo ni mafupisho yanayounganisha vifupi vya jina asilia "W"izard of "Oz".

Hata kama mwanzoni haikupokelewa vizuri sana iliendelea kuvuta watazamaji ikaendelea kwa miaka 4 hadi 1979 na kuonyeshwa mara 1,672.

Filamu yake ilitolewa 1978 kwa pamoja na Universal Pictures and Motown Productions ikiongozwa na Sidney Lumet. Kati ya waigizaji walikuwepo Diana Ross, Michael Jackson, Theresa Merritt, Thelma Carpenter, Lena Horne, Richard Pryor na Nipsey Russell.