Tianjin (kwa Kichina: 天津), ni mji mkubwa katika China kaskazini.

Tianjin
天津市
Tianjin Financial Center na Mto Hai, Kanisa Kuu la Mt. Yosefu, kitovu cha jiii, Kituo cha reli Tianjin, "Jicho la Tianjin"
Nchi China
Jimbo / Mkoa (chini ya serikali kuu)
Anwani ya kijiografia Coordinates: 39°08′N 117°11′E / 39.133°N 117.183°E / 39.133; 117.183
Eneo km2 11,946
Wakazi 15,621,200
Msongamano wa watu 1,300/km2
Simu 22

Idadi ya wakazi ni 11,760,000 wanaoishi kwenye eneo la kilomita za mraba 11,917.

Mji huu ulianzishwa mwaka 1403 na kaisari Yongle kilomita 137 kutoka Beijing karibu na mdomo wa Mto Hai katika Bahari ya Bohai.

Tasnia ya kisasa ya mitambo na nguo ya China ilianza hapa. Tangu mwanzo wa Sera ya Mlango Wazi mwaka 1984, Tianjin iliongezwa maeneo mengi ya viwanda. Tangu 1994 hadi 2008, kiwango cha pato la taifa cha Tianjin kiliongezeka asilimia 12.5 kwa wastani kila mwaka.

Tianjin ni pia mahali pa kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kwanza nchini China kwenye mwaka 1895. Mji huo una taasisi karibu zaidi ya elfu za sayansi na teknolojia, pamoja na wataalamu zaidi ya elfu 600 katika fani tofauti. Inayo idadi kubwa ya wataalamu maarufu na wasomi.

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

  Tianjin travel guide kutoka Wikisafiri

  Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tianjin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.