Triti (pia tritiumu[1], ing. Tritium) ni isotopi nururifu ya hidrojeni yenye masi atomia 3.016. Triti ina protoni moja na nyutroni mbili. Kiini cha hidrojeni ya kawaida haina nyutroni bali protoni moja tu. Alama ya Triti ni 3H bali T hutumiwa pia.

Katika mazingira asilia triti hutokea kwa kiasi kidogo sana kutokana na mnururisho kutoka anga-nje unapopasua atomu za nitrojeni hewani. Triti nu nururifu na nusumaisha yake ni mnamo miaka 8 tu hivyo inapotea haraka. Triti inatengenezwa katika tanuri nyuklia kwa matumizi mbalimbali.

Kuna isotopi nyingine ya hidrojeni inayoitwa duteri yenye nyutroni moja.


Tanbihi hariri

  1. "Triti" inafuata muundo wa istilahi za KAST, "tritiumu" ni pendekezo la KSBFK