Tula
Tula (Kirusi: Тула) ni mji wa Urusi ya Kati wenye wakazi 509,000 hivi ulioko kilomita 200 kusini kwa Moskva. Iko katika mkoa wa Tula Oblast.
Tula ina historia ndefu ya miaka 850 ikatajwa mara ya kwanza katika hati ya mwaka 1146.
Kuna majengo ya kihistoria, kama makanisa na boma la Kremlin, yaliyodumu hadi leo.
Watalii wanaotembelea Tula wanaelekea Yasnaya Polyana, kilomita 14 upande wa kusini, alikoishi mwandishi mashuhuri Lev Tolstoy aliyezikwa hapa pia.
Leo hii ni mji wa viwanda hasa vinavyotengeza silaha na pia mashine mbalimbali.
Picha za Tula
hariri-
Ukuta wa kremlin
-
Mnara wa kremlin
-
Kanisa Kuu
-
Makumbusho ya silaha za Tula
-
Kituo cha reli cha Moskovski
-
Kiwanda cha silaha
-
Jumba la manisipaa
-
Mto Upa
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu: