Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (kwa Kiingereza National Electoral Commission au NEC) ni tume ya uchaguzi nchini Tanzania.[1]

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania ilianzishwa mwaka 1993 na Ali Hassan Mwinyi, rais wa pili wa Tanzania baada ya kuundwa kwa tume ya kukusanya maoni ya Tanzania kubaki katika mfumo wa chama kimoja au kuingia katika mfumo wa vyama vingi, tume iliyokuwa ikiongozwa na jaji Francis Nyalali mwaka 1991.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa chini ya ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Wajumbe wa Tume waliteuliwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 Januari 1993. [2]

Marejeo hariri

  1. "Constitution of Tanzania". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 April 2015. Iliwekwa mnamo 2 May 2015.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. https://www.nec.go.tz/pages/how-nec-is-established