Tunzaa ni aplikesheni ya kuimarisha tabia chanya za matumizi ya kifedha kwa vijana wa Kitanzania kupitia teknolojia ya simu za mkononi. Ilianzishwa mwaka 2019 na makao makuu yake yapo Dar es Salaam, Tanzania.

Lebo rasmi ya Tunzaa
URLtunzaa.co.tz
Biashara?Ndio
Aina ya tovutiAplikesheni ya Simu
Lugha zilizopoSwahili
MmilikiTunzaa Fintech
SasaActive

Historia hariri

Tunzaa ilianzishwa mnamo 2019 na Ng'winula Kingamkono[1]. Hapo awali ilifanya kazi kama muuzaji wa bidhaa mtandaoni kwa Dar es Salaam tu na ilizingatia zaidi vifaa vya kieletroniki na vyombo vya nyumbani, lakini ikapanua wigo wake kwa Tanzania nzima mnamo 2021 na hatua kwa hatua ikapanua wigo wake wa aina nyingine za bidhaa na huduma.

Hivi sasa watumiaji wa Tunzaa wanapata bidhaa na huduma kutoka kwa wafanyabiashara kuanzia vifaa vya nyumbani, safari, runinga, mashine za kufulia, friji, simu za mkononi, kompyuta na nyinginezo zinazowapa watumiaji njia rahisi ya kulipia huduma na bidhaa na kufuatilia matumizi yao.[2]

Aina za huduma hariri

Inawezesha malipo ya bidhaa na huduma kwa kiwango kidogo cha pesa kwa kasi ya mtumiaji mwenyewe moja kwa moja kutoka kwenye simu yake.[3]

Inawapa watumiaji uwezo wa kufuatilia kila pesa wanayoweka kando kwa lengo maalum kwa wakati halisi, kwa mfano kununua TV mpya, au simu ya hivi karibuni au kusafiri kwenda Zanzibar).[4]

Soko la Tunzaa hariri

Soko la bidhaa na huduma la Tunzaa linaruhusu wafanyabiashara nchini Tanzania kuuza bidhaa zao mtandaoni. Watumiaji wa Tunzaa wanapata bidhaa na huduma kutoka kwa wafanyabiashara kuanzia vifaa vya nyumbani, safari, runinga, mashine za kufulia, friji, simu za mkononi, kompyuta na nyinginezo zinazowapa watumiaji njia rahisi ya kulipia huduma na bidhaa na kufuatilia matumizi yao[5].

Marejeo hariri

  1. "Tunzaa Fintech launches platform that develops positive financial habits in young people". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-11. 
  2. "Tunzaa yazindua App ya kuimarisha tabia za kifedha kwa wanunuaji na wauzaji wa huduma na bidhaa". Swahili Times (kwa en-US). 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-08-11. 
  3. "Tunzaa yaja na muarobaini matumizi bora ya fedha kwa wanunuaji na wauzaji wa huduma na bidhaa". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-11. 
  4. Pascal Mwakyoma TZA. "Mtanzania ameleta App ya kuimarisha tabia za kifedha kwa wanunuaji na wauzaji – Millard Ayo TV". millardayo.com (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-08-11. 
  5. "Tunzaa Fintech launches platform that develops positive financial habits in young people". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-11. 

Viungo vya nje hariri